NA ADSON KAGIYE |
Fursa nyingi huja na kutoweka, zingine hudumu kwa kitambo,
zingine hudumu kwa karne. Mfano soda ya cocacola imekuwa Sokoni tangu
mwanzo mwa karne hii.
Fursa huenda na utayari wa MTU, ni kama mbegu, ukipanda
kwenye mwamba wenye Maji itaota lakini haitakuwa na kuzaaa, ukipanda
kwenye pori itaota na kukua na kutoa mazao hafifu na ukipanda kwenye
udongo mzuri inaota na kuzaa.
Na ndio mana utasikia ukifa maskini ni kosa lako mwenyewe
kwa kuwa ulikuwa hujajiandaa kuipokea fursa, hukuandaa mazingira mazuri
ya kuipokea fursa, hukuwa tayari kuitunza fursa na wakati wa mavuno
ulipokaribia uliwaachia ndege wale mavuno yako
HATARI KUBWA SI KUTOKUONA FURSA Bali ni kutokujiandaa
kuiona fursa. Yaani unakuta mtu anaziba masikio yake hataki hata
kuelezwa fursa yeyote.
Kama cocacola wasingeweza kuona fursa ktk soko la vinywaji,
wakspambani kutengeneza brand yao na kuwa mstari wa mbele ktk jamii
basi Leo hii usingeisikia cocacola Tanzania.
JE UKIPEWA FURSA UTAIFANYIA KAZI, AU UTABAKIA KUSEMA NIPO BIZE?
Na Adson Kagiye
Na Adson Kagiye
Post a Comment