Na Ferdinand
Shayo,Arusha.
Shirika la
Hifadhi za Taifa TANAPA limejipanga kuzindua kampeni ya kitaifa ya kufanya usafi mlima Kilimanjaro ambao
unakusanya mapato ya shilingi bilioni 60 kwa mwaka na kuajiri Watanzania laki
3.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na
Waandishi wa Habari amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuboresha mazingira safi
ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuinusuru na uchafuzi wa mazingira wa
kidunia (Global warming), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), inatarajia
kuzindua kampeni ya usafi wa mlima Kilimanjaro kesho ambayo itadumu kwa siku
kumi.
“Tumeamua
kufanya usafi katika mlima huo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais
John Pombe Magufuli katika kuweka mazingira katika hali ya usafi hususan hifadhi
za taifa” Alisema Shelutete
Katibu Mkuu
wa Chama cha Mawakala wa Utalii Sirili Akko amesema kuwa mashirika binafsi
yaliyoko kwenye sekta ya utalii hayana budi kushiriki katika kufanya usafi
katika mlima huo wa kwanza kwa urefu barani Afrika na wapili duniani.
Pia ameitaka
serikali kusimamia maagizo ya Ofisi Makamu wa Raisi Mazingira kwa kupiga
marufuku ya matumizi plastiki katika hifadhi za taifa ili kuepuka kuchafua
mazingira.
Mdau wa Masuala
ya Utalii ambaye ni Afisa Masoko wa Hoteli ya Kibo Palace Jenipher Swai amesema
kuwa wameungana na Tanapa kufanya usafi kwa kutoa vifaa vya kufanyia usafi
pamoja na kushiriki kupanda mlima huo katika madhimisho ya miaka kumi ya
kuanzishwa kwa hoteli hiyo.
Jumla ya
Watalii 50000 hutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro na kuchangia shilingi
bilioni 60,kampeni ya kufanya usafi ya muda wa siku 10 itanza kesho
ikiwashirikisha wapagazi,waongoza watalii na wadau wa utalii ,kuhakikisha hali
ya usafi katika hifadhi zetu zitasaidia kuvutia watalii zaidi.
Post a Comment