PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAASISI YA WANAUME JIJINI ARUSHA YALAANIVITENDO VYA USHOGA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume...
Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.Picha na Ferdinand Sh

Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.Picha na Ferdinand Shayo

Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.Picha na Ferdinand Sh


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Taasisi isiyo ya  kiserikali ya Wanaume Kazini maarufu kama Man at Work imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi na thamani ya wanaume hivyo wameitaka serikali kupiga vite vitendo hivyo ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.

Muasisi wa Taasisi hiyo  yenye makao yake jijini Arusha Maxwell  Stanslaus  amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha Mara moja.

Maxwell alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katinga ngazi ya familia,jamii na taifa ili kuchochea maendeleo.

“Kwa sasa tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu yake hivyo Basi  Wanaume zaidi ya Milioni  walioko Tanzania wakiamua kutimiza majukumu yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema  Maxwell

Moja kati ya Wanaume waliohudhuria ni Joseph Mayagila alisema kuwa matatizo ya ushoga yanatokana na baadhi ya wanaume kujisahau na kujaribu kuwa wanawake ,jukwaa hili la wanaume ni muhimu kuwakumbusha wanaume juu ya uanaume wao na kutimiza yale yanayowapasa kama wanaume.

Dokta Emmanuel Buganga  ameeleza kuwa vuguvugu la wanawake kudai haki zao linatokana na baadhi ya wanaume kutotimiza wajibu wao kama wanaume wameacha majukumu yao ya kutunza familia zao na kuwa walezi na walinzi wa familia .

Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali amesema kuwa wanaume wengi wamejisahau sana katika masuala ya malezi ya familia kwani usimpolea mtoto katika njia impasayo atakuja kukuaibisha ukubwani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top