PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MTAZAMO HASI UNAVYOKUZUIA KUINGIA KWENYE MAFANIKIO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Njia mojawapo ya kushinda ni kuondoa mawazo ya kushindwa kwenye kila jambo la kimafanikio unalotaka ku...


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Njia mojawapo ya kushinda ni kuondoa mawazo ya kushindwa kwenye kila jambo la kimafanikio unalotaka kufanya.

Watu wengi wanashindwa kufanikisha maisha yao ya kiuchumi ,kijamii na kibiashara kwasababu ya kutawaliwa na mawazo ya kushindwa yamekua mengi kuliko mawazo ya kushinda katika akili na mawazo yao.

Hili ni Tatizo kubwa  duniani ambalo limekua likizuia mafanikio ya watu wengi na kufanya ndoto nyingi zife.

Mawazo ya kushindwa na mtazamo hasi ni kama bomu ambalo linasambaratisha mawazo mazuri aliyoyanayo mtu,ndoto na maono.

Kumbuka kuwa wazo zuri moja ulilonalo ukilifanyia kazi linaweza kukupa mafanikio makubwa na maisha mazuri unayoyataka.

Fikiri juu ya mawazo mabaya uliyonayo yanakupa nini katika maisha yako sana sana yanakupa kushindwa katika  mambo mengi ya kimafanikio unayojaribu kuyafanya.

Inatupasa kuwekeza kwenye kuwaza vizuri,kufikiri vizuri ili tuweze kutenda vizuri na kufanikisha mambo yetu.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa mtu ni matokeo ya mawazo yake maana yake jinsi unavyowaza ndivyo utakavyokua ,jiulize unawaza nini?

“Mawazo mazuri yanaweza kutengeneza maisha yako na mawazo mabaya yanaweza kuyaharibu maisha yako”

Kumbuka kila kitu unachokiona duniani kilikua ni mawazo ya watu na ndoto zao kama vile kompyuta,simu,gari,mavazi,majengo makubwa kwa madogo na vitu vingine vingi.

Jiulize kuwa una mawazo gani ambayo yanaweza kukufikisha kwenye mafanikio  unayoyataka na kukupa maisha unayoyataka.

Yatupasa kuwekeza kwenye mawazo yetu na fikra zetu ,kutengeneza mitazamo chanya itakayokufikisha kwenye mafanikio.

Mtazamo  ni kama msingi wa nyumba ,ukiwa na msingi mbovu nyumba haiwezi kusimama hata kama inapakwa rangi nzuri  kiasi gani lazima itaanguka tu na kwa binadamu ni hivyo hivyo.

Uwe na uhakika kuwa ukiwa na mtazamo hasi utaanguka tu haijalishi unavaa suti ,una pesa kiasi gani kwa sababu mtazamo ni msingi.

Ukitaka kutengeneza mtazamo chanya inakupasa inakupasa kuepuka kukaa na watu wenye mtazamo hasi watu ambao wamejaa mawazo ya kushindwa .

Watu ambao ukiwaambia jambo wanakukatisha tamaa watu ambao wameshindwa kabla hata hawajaanza kutokana na mtazamo wao hasi.
Kaa mbali na watu kama hao ukitaka kufanikiwa  maana “Ukitaka kupaa kama Ndege aina ya  tai  tafuta marafiki ambao wanapaa kama tai usikae na marafiki wanaoiashi kama kuku kupaa kwako itakua ndoto utabaki kuishi maisha ya chini.

Tazama vipindi vya runinga,redio na magazeti ambayo yanakupa hamasa na ari ya kutimiza ndoto zako  vitu ambavyo vinakujenga zaidi  na si kukuharibu .

Usijaze habari za mauaji,ukatili kwenye kichwa chako jaza vitu ambavyo vitakupa afya za kusonga mbele  na kutimiza ndoto zako.

“We became what we think” maana yake Tunakua vile tunavofikiria .Ni vyema  kujizuilia kufikiria vibaya juu yako na kuwafikiria vibaya wengine ili kutengeneza mtazamo chanya.

Jitaidi sana ukionyeshwa donate usione tundu uone donati  na huo ndo mtazamo chanya  hata katika giza unaweza kuona mwanga kutokana na mtazamo wako na katika matatizo unaweza kuona suluhu kutokana na mtazamo wako.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa akili  yako ni kama benki utakachokiingiza ndicho utakachokitoa  akionyesha umuhimu wa kuwa makini na vitu tunavyoviingiza vichwani mwetu.

“Your Mind is like a Bank what you Deposit is what you Withdraw”

Kuwa makini na kila unachokiingiza kichwani kwako,Nakutakia mafanikio kwenye maisha yako


0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top