Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Hospitali ya Ngarenaro inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya
kuhudumia wagonjwa pamoja na kukosekana kwa miundombinu imara ya maji katika
chumba cha upasuaji hivyo kuhitaji upanuzi pamoja na ukarabati wa hospitali
hiyo ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000 wa kata ya Ngarenaro jijini
Arusha.
Akizungumzia changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali
hiyo Josephat Kivuyo katika taarifa yake
kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa hospitali hiyo inahitaji
upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha huduma za afya ambazo zinahitajika na
wananchi wengi.
Daktari huyo Mfawidhi alisema kuwa changamoto nyingine ni
uhaba wa magari ya wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la
zamani na haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wananchi na wadau mbalimbali
kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya ukarabati ambao tayari
umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa wananchi na wahudumu wa afya.
Pia Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa
wagonjwa na kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya
ambayo inahudumia watanzania wengi.
Alisema Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na
tayari hivyo nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika
kuhakikisha kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma
za afya.
Post a Comment