Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa
Majambazi watatu yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa
jina la Emmanuel Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo
yalianza kujibizana risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha
polisi na kufika katika eneo la tukio.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita
Kawawa, amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na
majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku
akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Akizungumza kwa njia ya simu kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani
Shinyanga ACP Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi punde
wanapoona dalili zozote za kiuhalifu zinafanyika.
Katika tukio hilo jeshi polisi limefanikiwa kukamata bunduki mbili moja
aina ya Short Gun na moja ya kivita aina ya Uzgun, bomu la kutupa kwa
mkono, kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na magazine mbili
za bunduki.
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment