MWENYEKITI
wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama amekoshwa
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuwa mgeni
rasmi kwenye Tamasha la Pasaka litakalofanyika Mwanza Machi 27 na
kueleza kwamba ni faraja kwao.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya
tamasha hilo, Alex Msama alisema Nape ni mmoja wa walezi wa tamasha hilo
ambalo mwaka huu linatarajia kuanzia Geita Machi 26 na kumalizikia
Kahama Machi 28.
“Maandalizi
kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema na mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa waziri Nape, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae
kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa
muziki wa Injili,” alisema Msama na kuongeza.
“Tunafurahishwa
na Waziri Nape kukubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwa
sababu ni mmoja wa wanaoweza kusaidia mipangilio ya Matamasha
yanayoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions kama ilivyokuwa Tamasha la
Krismasi lililofanyika mwaka jana,” alisema Msama.
Aidha
Msama anatumia fursa hiyo kuwaweka bayana waimbaji waliothibitisha
kushiriki Tamasha la Pasaka ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny
Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua
Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro ya
Mwanza na Kwaya ya Wakorintho wa pili kutoka Njombe.
Anavitaja
viingilio katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa ni
Sh. 5,000 kwa wakubwa na kwa watoto Sh 2,000. Msama alisema maandalizi
ya tamasha hilo yanaendelea vema na kutoa wito kwa wakazi wa mikoa ya
Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi.
Post a Comment