Mwenyekiti
wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango
Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano
inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo
Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari
watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige
kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam.
Umoja
wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho)
unataraji kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa watoto walio na umri
chini ya miaka mitano, upimaji utakaofanyika Jumapili ya Machi, 13
katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumzia
huduma hiyo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee amesema huduma
hiyo itawawezesha wazazi kutambua magonjwa yanayowakabili watoto wao
bila kulipa malipo yoyote kwa kutambua umuhimu wa afya ya watoto kwa
maendeleo ya taifa.
Alisema
kupitia huduma hiyo madaktari watawapima watoto walio na umri chini ya
miaka mitano afya ya kinywa, uzito, ukaguzi na ushauri wa lishe hivyo
kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata huduma bure.
Mmoja
wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt.
Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam akifafanua
jambo kuhusiana na umuhimu wa kupima afya za watoto katika mkutano na
waandishi wa habari.
“Tunataka
kusaidia marafiki zetu wa Tanzania na katika kuendelea hilo tutatoa
huduma ya bure kwa watoto kupima afya zao na tunataka wazazi wawalete
watoto ili wapime afya,” alisema Banerjee.
Nae
Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki Al Hilal alisema Bango Sangho kimekuwa
chama ambacho kikisaidia jamii ya Tanzania katika sekta ya afya na
wamekuwa wakitoa huduma ya kupima watoto bure walio na umri chini ya
miaka mitano kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Alisema
ripoti ya afya Tanzania inaonyesha kuwa kuna watoto 81 wamekuwa
wakipoteza maisha kati ya watoto 1,000 walio na umri chini ya miaka
mitano kutokana na sababu mbalimbali ambapo wamekuwa hawapati huduma na
kupitia huduma hiyo ya kuwapima bure watoto walio na magonjwa wataweza
kutambulika.
“Tutafanya
huduma ya kupima bure watoto walio chini ya miaka mitano na
tutakaobaini wanamatatizo maalum ya kiafya tutawapa rufaa ili wakapate
huduma ya matibabu,” alisema Dkt. Mzige.
Huduma
hiyo ya kupima watoto walio na umri chini ya miaka mitano ilifanyika
pia mwaka jana na watoto 289 walipimwa afya zao huku baadhi walikutwa na
matatizo ikiwemo maambukizi ya mfumo wa njia ya mkojo UTI, Utapiamlo,
kukatwa vimeo na wengine wakionekana kuwa na afya duni.
Mtaalamu
wa afya ya uzazi kutoka Kliniki ya Al Hilal, Bi. Husna Abdallah akitoa
msisitizo kwa akina mama kuzingatia kanuni za afya ya uzazi wakati wa
mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Post a Comment