Na Woinde Shizza,Simanjiro
Mpango mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la awali mpaka
sekondari umeonekana kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno
hususani jamii ya kifugaji kutoka katika
kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua
kumkodisha mwalimu na kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.
Wanafunzi wa shule
hii ya msingi Kichagare wamekuwa
wanajisomea wakiwa wamekaa chini huku shule hiyo ikiwa imeezekwa na vipande vya turubai ili kuweza kupata
ahueni wakati wakujisomea ambapolengo la wazazi wao kufanya hivyo ni kuwasaidia
watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na karne hii ya sasa ya
teknolojia.
Gazeti hili lilibahatika kufika eneo la tukio na kuzungumza
na mwalimu wa shule hiyoaliyejitambulisha kwa jina la Lilian Nanyaro ambapo alisema kuwa aliamuakujitolea
kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare kitongoji cha Loongung hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia
wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .
Alisema kuwa mazingira
ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika swala zima la ufundishaji
kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo ukizingatia kwamba watoto ambao ni wanafunzi wana nia ya kutaka kusoma.
‘’ndugu mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu
hamna paa paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka na pia ukiangalia mazingira ya kijiji chetu
mvua zinaponyesha pia inakuwa ni tatizo kubwa sana kwani inafikia mahali wanafunzi hushindwa kufika shule kabisa
nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza kutusaidia tatizo hili
kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya kusomea itawasadia sana
hivo wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema
Nanyaro.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo
aliyejitambulisha kwa jina la Seigulu James
alisema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma lakini tatizo
kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana ,kwani
kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.
Alitumia fursa hiyo kuiomba serekali kuwasaidia kuweza
kupata angalau madawati pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na
kuwapatia walimu ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama
wanafunzi wengine na watoto wa
shule zingine.
Honie Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani
Simanjiro alisema kuwa wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu
mmoja ambaye ndio wanae hapo shule ambapo alisema wao kama wanakijiji
wanajichangisha ela na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.
“sisi tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute
mwalimu ambaye atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo
tunajichanga tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia
shilingi elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet
Losijake alisema kuwa mapaka sasa tayari
vikao vyao vya bajeti halmashauri
wameshaomba kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu
wa darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.
Post a Comment