Na Ferdinand Shayo,Mwanza .
Uvuvi haramu wa kutumia sumu kali,pamoja na neti umekua
ukitishia uhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Saa Nane na Lubondo ambazo
zimepewa jukumu la kulinda mazalia ya samaki ili samaki hao wasipotee kwenye
uso wa dunia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofanya
ziara ya kutembelea hifadhi hiyo ya Saa Nane iliyoko jijini Mwanza ,ziara iliyoratibiwa na
Tanapa Mhifadhi Mkuu Donatus Bayona amesema kuwa changamoto inayowakabili ni
uvuvi haramu na uvamizi wa maeneo ya hifadhi unaofanywa na wavuvi wanaojipatia
kipato bila kujali kuwa wanaharibu mazalia ya samaki .
Askari Wanyamapori katika hifadhi hiyo Aloyce Mong`ee
amesema kuwa wamekua wakiimarisha
doria katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia shughuli hizo za uvuvi ambazo ni
tishio kwa uhifadhi.
“Kuna mipaka ambayo tumeweka hakuna mtu anayeruhusiwa
kufanya uvuvi ndani ya eneo la hifadhi ili kuhifadhi mazalia ya samaki” Alisema
Askari huyo
Mhifadhi huyo amesema kuwa Hifadhi hiyo ambayo iko katikati
ya jiji la Mwanza inaongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani ambao ni
asilimia 90% ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Alisema Hifadhi ya
Saa Nane ni moja kati ya hifadhi zilizopo kati kati ya miji hivyo kuvutia
watanzania wengi kutembelea eneo hilo
ambali lina wanyama pori pundamilia,swala na sokwe weusi pamoja na madhari nzuri
na maridhawa ambazo hutumika kama sehemu ya kujifunzia na kupumzikia.
Post a Comment