Jana usiku March 03,2016 ulikuwa ni Usiku wa Miss DEBORA JACKSON ROSKA MKAMA (kushoto) mkazi wa Lumala, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Ulikuwa ni Usiku maalumu kwa ajili ya Miss Debora kwa ajili ya SENDOFF PARTY iliyofanyika katika Ukumbi wa Ebeneza ulioko katika Kanisa la KKKT Iloganzara Manispaa ya Ilemela.
Miss Debora anatarajia kufunga Pingu za Maisha na Mwanahabari na Mtangazaji wa Radio Storm Fm ya Mkoani Geita, JOEL MADUKA, siku ya kesho March 05,2016 katika Kanisa la AICT Igoma Jijini Mwanza na baadae sherehe kuhamia katika Ukumbi wa Mwanza Youth Centre uliopo Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Mwenye Kinasa sauti pichani juu ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sendoff akiwakaribisha Waalikwa.
Mwenye Kinasa sauti ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Ilemela Mkoani Mwanza Dkt.Daniel Kulola akimkaribisha bibi harusi Mtarajiwa pamoja na wageni waalikwa kwa maombi.
Bibi harusi Mtarajiwa Debora Jackson akikata utepe kuingia Ukumbini
Kushoto ni bibi harusi mtarajiwa akiingia ukumbini kwa madaha akiwa pamoja na msimamizi wake
Kulia ni Bibi harusi mtarajiwa akijiandaa kukata keki
Kwa heshima na nidhamu kabisa, Bibi harusi Mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake Upande wa Bwana harusi
Kwa heshima na nidhamu kabisa, Bibi harusi Mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake Upande wa bibi harusi
Bibi harusi mtarajiwa (Kulia) akiwa pamoja na msimamizi wake
Ndugu wa bibi harusi, Joram Samweli akifungua Shampain kwa madaha kabisa
Bibi harusi mtarajiwa (kulia) akiwa pamoja na msimamizi wake tayari kwa kuonja shampain
Wageni waalikwa wakigonga cheers na bibi harusi mtarajiwa
Wageni waalikwa wakigonga cheers na bibi harusi mtarajiwa
Wageni waalikwa wakigonga cheers na bibi harusi mtarajiwa
Muda wa bibi harusi mtarajiwa, kumtafuta mpendwa wake sasa
Huyooooooooo, mpendwa kapatikana. Ni Joel Maduka (Kushoto) akiwa na bibi harusi mtarajiwa (kulia)
Cheers kwanza
Bibi harusi mtarajiwa akiwa na bwana harusi mtarajiwa katika kuchukua msosi
Ni upendo wa dhati
Mzazi wa bibi harusi akitoa nasaha kwa bibi harusi mtarajiwa
Debora akawaambia "Msinikawize, mradi Bwana amefanikisha njia yangu, nipendi ruhusa niende kwa bwana wangu".
Bonyea HAPA Kutazama picha za Kuvishwa Pete.
Imeandaliwa na Binagi Media Group.
Post a Comment