PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TETESI: Clouds FM Kuwatema Baadhi ya Watangazaji...PJ na Gerald Hando Watajwa
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Habari zinasema kwamba PJ, Abel Onesmo na Gerald Hando watapigwa chini kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa kawaida, Clouds w...


Habari zinasema kwamba PJ, Abel Onesmo na Gerald Hando watapigwa chini kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa kawaida, Clouds wana utaratibu wa kutoa mikataba mipya kila ifikapo April 1.

Katika zoezi hilo kuna wafanyakazi wapya wanaopewa mikataba na wale wa zamani ambao kituo kinawahitaji "hurenew" mikataba yao.

Imefahamika kwamba PJ , Abel Onesmo na Gerald Hando ambao wote wanatoka kipindi cha Power Breakfast (PB) watapigwa chini mwezi huu au kwa kauli ya mjini ni kwamba "Watatumbuliwa".

Sababu kubwa inayotajwa ya wakongwe hao kupigwa chini ni kushindwa kuendana na taratibu za kampuni hiyo kongwe na kinara katika sekta ya Burudani nchini kwani wanajiona wao wako juu ya watu wote.

Pia inasemekana suala la Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 limewauma sana kwani walikuwa wanaamini wao ndio kipindi bora zaidi cha asubuhi hivyo Suala la Magufuli kupiga simu 360 limeprove "otherwise".

Inadaiwa kuwa msuguano mkubwa ulianza wakati wa kipindi cha uchaguzi kutokana na kutumika kisiasa na kulipwa na baadhi ya wanasiasa ili watumie Power Breakfast kama jukwaa la kuwasafisha kinyume na maadili ya kazi yao yanayosisitiza "neutrality" katika kutoa habari.

Vilevile habari za kuaminika kutoka ndani ya Clouds zinasema kwamba tayari Clouds Media Group imeajiri vichwa vipya ambavyo kuanzia tarehe 1 vitaanza kupiga kazi.
CREDIT: UDAKU SPECIAL

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top