Jeshi
la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mwanamke mmoja Magreth Mosha
mkazi wa Kibaha mkoani Pwani kwa tuhuma ya kupatikana na vipande saba
vya meno ya tembo.
Jeshi
hilo pia linamshikilia Bw. Hamis Balewa mkazi wa kijiji cha Mbasa
wilayani Malinyi kwa kukutwa na nyama ya sheshe kilo ishirini zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Morogoro SACP Urich Matei amesema
watu hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti ambapo tukio la
kwanza limetokea katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo katika
manispaa ya Morogoro ambapo akiwa na vipande saba vya meno ya tembo.
Katika
hatua nyingine watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo
katika matukio tofauti wakiwemo watumishi watatu wa shirika la ugavi wa
umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo baada ya mfanyakazi mwenzao Deo
Elias kufariki dunia baada ya kunaswa na umeme wakati akiwa kazini .
Akizungumzia
matukio hayo kamanda wa polisi Urich Matei amesema katika tukio la
kwanza watu wawili wakazi wa jijini Dar-es-salaam bw. Arisha Shaaban na
Bi Zainabu Athuman wanashikiliwa kwa kukutwa na debe sita za bangi huku
wafanyakazi watatu wa shirika la TANESCO Bw Ramadhani Yusuf, Bi
Elizabeth Kihimbo na Bw Jonas Sajinga wakishikiliwa kuhusiana na kifo
cha mtumishi mwenzao.
Watuhumiwa
wote wanaohusika na matukio hayo wanatarajia kufikishwa mahakamani
kujibu mashtaka yanayowakabili mara baada ya upelelezi wa jeshi hilo
kukamilika.
Post a Comment