Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Millard Ayo baada ya kufungua studio yake kubwa naya kisasa jijini Dar, ameanza kuuza vipindi vya burudani katika radio mbalimbali za Afrika Mashariki.
millard
Akizungumza Jumamosi hii katika mdahalo wa kuwatia moyo wanafunzi waliofeli kidato cha nne, ambao ulienda sambamba na uzinduzi wa video mpya ya Mrisho Mpoto, Millard alieleza mafanikio yake baada ya kupambana kwa muda mrefu.
“Nilijiuliza kwanini nisitumie uandishi wangu wa habari ili kusambaza habari Afrika?, ndipo nikaanza kujinyima ili nijenge studio yangu kwa pesa yangu mpaka imekamilika. Sasa hivi tayari nimeshaanza kuuza vipindi vyangu katika radio mbalimbali za Afrika, Kenya, Rwanda. Pia nimekuwa reporter wa radio mbalimbali za Afrika Mashariki, pia Nigeria kuna kazi maalum nimepata ambayo nimehifurahia sana,” alisema Millard.
Aliongeza, “Nimeona kama Rwanda na Kenya sasa hivi bongofleva ndiyo imetake over, hawa watu ingawa wanasikiliza muziki, pia wanataka stori mbalimbali za mastaa wa bongofleva. Kwa hiyo mimi nataka kuwaambia watu wangu tusikate tamaa kama ulianguka inuka endelea,”
Pia Millard Ayo alisema yeye ni miongoni mwa wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne lakini aliinuka na kuendelea.
Post a Comment