Umaarufu wake ulichangiwa zaidi na mahusiano yake ya kimapenzi na watu maarufu kuanzia TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Diamond na hivi karibuni, mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan. Lakini niseme kuwa uhusiano wake na Diamond ndiyo uliomulikwa zaidi kuliko mwingine wowote.
Ni katika uhusiano wao, jina la Diamond lilivuma zaidi hasa kwakuwa kipindi wanaanza, Wema alikuwa tayari kwenye kilele cha umaarufu, na hitmaker huyo alikuwa ameanza kuikwea ngazi.
Kwa kipindi chote hicho, Wema amekuwa ni brand kubwa. Wema ni mgodi unaotembea. Hii ni kwasababu hakuna staa mwingine wa kike Afrika Mashariki mwenye kundi kubwa zaidi la mashabiki nyuma yake. Ni kundi kubwa ambalo lipo tayari kumtetea na kumpigania katika nyakati zote, mbaya au nzuri.
Kundi hili limeendelea kuwa aminifu kwake hata pale anapoanzisha uhusiano na mtu mwingine. Lilikuwa nyuma yake kipindi yupo na Diamond na hadi walipoachana. Limeendelea kumfuata kipindi ameanzisha uhusiano na Idris kiasi cha kuifanya couple hiyo itengeneze headlines nyingi ndani ya muda mfupi.
Kwahiyo kwa namna yoyote ile, Wema ni brand inayoweza kuingiza fedha nyingi. Japo alitakiwa kuwa mbali sana kutokana na ushawishi alionao, nafurahi kuona kwamba tayari ameigundua thamani yake na kuanza kuitumia. Napenda kumuona Wema huyu wa sasa ambaye akili yake imefocus zaidi kibiashara na kupush brand yake ya lipstick, Kiss by Wema Sepetu.
Napenda ninavyoona anavyotumia nguvu kuisambaza na kutafuta mawakala nchi nzima. Ninachofurahia zaidi ni kuona kuwa anaisambaza hadi Kenya ambako kuna mashabiki wake wengi sana. Lipstick zake zipo katika rangi mbalimbali na kwa muonekano wa picha ninazoziona, zinaonekana ziko poa.
Cha msingi sana mashabiki wake wa kike na hata wanawake wengine tu wanaopenda urembo, wamuunge mkono kwa kununua bidhaa za mzawa. Ni kwa kufanya hivyo ndivyo tunavyoweza kutengeneza mastaa ambao hawaiishi kuwa na majina tu, bali pia wanakuwa na uwezo kifedha. Naamini huu ni mwanzo wa Wema kuliwekea thamani jina lake na kutengeneza bidhaa nyingi zaidi sababu wateja wapo.
Leo ameanza na lipstick, kesho anaweza kuja na perfume, lotion, mafuta na bidhaa zingine kibao. Cha msingi napenda kuona akiendelea na mzuka huu wa kupush brand yake yeye mwenyewe kwa nguvu zote. Ni hivi ndivyo wanavyofanya mastaa wa nje kama akina Diddy kupromote bidhaa zao.
Kwa kufanya hivi na kwa jitihada zake, haitachukua muda mrefu kampuni kubwa kuonesha interest ya kuwekeza mabilioni ya shilingi kwenye brand yake. Huyu ndiye Wema tunayempenda, na sio yule wa drama ambaye mwisho wa siku tumejikuta tukimpa jina The Drama Queen.
Source:Bongo 5
Post a Comment