Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mhandisi, Aloys Mtei (kulia) kuhusu
mabomba yanayotawanya mafuta kwenda kwenye matangi makubwa ya makampuni
mbalimbali kwenye eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam Februari 11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo ambalo mafuta hufunguliwa na
kufungwa ili kwenda kwenye matangi ya kuhifadhia mafuta ya makampuni
mbalimbali yanayoagiza mafuta toka nje ya nchi wakati alipokwenda eneo
la Kigamboni jijini Dar es salaam kuona mianya inayotumika kukwepa kodi
za mafuta yanayoagizwa nje ya nchikupitia bandari ya Dar es
salaam Februari 11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu
zilizomfanya azuie matumizi ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha
mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam wakati
alipofanya ziara kwenye badari hiyo Februari11, 2016. katikati ni Mkuu
wa Wilaya ya Ilala,Raymound Mushi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa na kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamla ya
bandari Tanzania, Mhandisi Aloys Mtei eneo zinakotia nanga meli kubwa
zinazoleta mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es salaam Februari 11,
2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo lenye mabomba yanayotumika
kupitisha mafuta kutoka kwenye meli kupitia bandari ya Dar es slaam
wkatia lipofanya ziara ya kukagua miundombinu yenye mianya ya ukwepaji
kodi hasa kwenye mafuta yanayoingia nchini Februari 11, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujezi na Uchukuzi, Profesa Makame
Mbarawa (kulia) wikimsikiliza Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania,Mhandisi, Aloys Mtei wakati alipotoa maelezo kuhusu uingizaji
wa mafuta kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam Februari
11, 2016.Mheshimiwa majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua miundombinu
yenye mianya ya ukwepaji kodi kwenye mafuta yanayoingia nchini kupitia
bandari hiyo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Flow Meter eneo la Kigamboni
jijini Dar es salaam Februari 11, 2016. Mtambo huo utatumika kupima
wingi wamafuta yanayotoka kwenye meli na kuingizwa hapa nchini. Kulia
kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymound Mushi.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post a Comment