Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawsiliaano Prof.Makame Mbarawa (Wa pili
kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja bishara wa kampuni ya Malaysia
inayojenga vichwa vya treni Srinivasan Rajmohan (Wa kwanza kulia) kuhusu
kufanya kazi hiyo kwa haraka ( Wa pili kushoto) ni katibu Mkuu Sekta ya
Uchukuzi Eng.Leonard Chamuriho na (Wapili kulia) ni Naibu Waziri
Eng.Edwin Ngonyani.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka
Makandarasi waliosimamisha kazi za ujenzi wa barabara nchini kuendelea
na ujenzi baada ya Serikali kuanza kuwalipa madai yao.
Akizungumza
mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu
wa kilomita 48.6 Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amesema
tayari Serikali imeshalipa makandarasi mbalimbali nchini shilingi
bilioni 400 na itaendelea kufanya hivyo ili kumaliza madeni yao kwa
haraka.
“Hakikisheni
mnarejea kazini na kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wenu katika
kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa ili ujenzi wa barabara na madaraja
ukamilike kwa mujibu wa mkataba na hivyo kuondoa usumbufu kwa watumiaji
wa barabara hii”, amesema Prof Mbarawa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia)
akimsikiliza Mbunge wa Mvomero Sadick Murad (kushoto) wakati akitoa
maelezo kuhusu ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani yenye urefu wa Km
48.6. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.
Profesa
Mbarawa amemhakikishia mkandarasi China Civil Engineering Construction
Corporation anayejenga barabara ya Magole-Turiani kuwa tayari serikali
imeshamlipa zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya laki 735 na
Shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 795 hivyo ni wakati wa
kukamilisha ujenzi huo hususan sehemu za madaraja kabla ya mvua za
masika kuaanza.
Akizungumza
katika ukaguzi huo Mbunge wa Mvomero Mhe. Sadick Murad ameiomba
Serikali kumalizia daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 ili liweze
kupitika.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua karakana ya ujenzi wa
vichwa vya treni mjini Morogoro na kumtaka mkandarasi anayekarabati
vichwa hivyo kufanya kazi hiyo kwa haraka na kutoa kazi nyingine kwa
watanzania ili kuwajengea uwezo wa kazi hizo.
Sehemu ya juu ya daraja la Diwale lenye urefu wa mita 75 likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake kama linavyoonekana.
Amewataka
wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kufanya kazi kwa ubunifu,
uadilifu na uwazi ili kufufua hadhi ya Shirika hilo ambalo ni muhimu
kwa uchumi wa nchi hii.
Amesema
takribani asilimia 96 ya mizigo inayoshushwa katika Bandari ya Dar es
salaam husafirishwa kwa njia ya barabara hivyo ni jukumu la TRL
kuhakikisha inapata mizigo ya kutosha ya kusafirisha ili kupunguza
mizigo hiyo kusafirishwa na barabara lakini kufufua uchumi wa TRL na
taifa kwa ujumla.
“Fanyeni
kazi kwa bidii, uwazi na kwa kushirikiana ili kujenga Shirika la Reli
la kisasa lenye uwezo wa kujitegemea acheni vitendo vya hujuma na migomo
vinavyoweza kudhoofisha shirika hili”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Mbunge
wa Mvomero Sadick Murad akimwongoza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) kuelekea katika daraja
la Diwale, wa tatu kulia ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng.
Dorothy Mtenga.
Naye
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani
amekemea vitendo wa wizi wa mafuta na kuhujumu Reli vinavyofanywa na
watumishi wasio waaminifu na kuwataka kuwa wazalendo kwa nchi yao ili
kuchochea kasi ya maendeleo.
Akizungumza
katika hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino
(Sekta ya Uchukuzi) Eng. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa
TRL Kuepuka migomo itakayoathiri utendaji wa Shirika hilo, kubuni
mikakati ya kuwezesha shirika hilo kujiendesha kwa faida, kupambana na
ubadhirifu wa mali na miundombinu na kufanya kazi kwa ushirikiano ili
kuleta tija inayokusudiwa.
Profesa
Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya kukagua utendaji wa taasisi zilizo
chini ya Wizara Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambapo amepata fursa ya
kukagua ujenzi wa mizani ya kisasa ya Mikese na kituo cha mtandao wa
mawasiliano ya simu vijijini ya Halotel unaosambazwa katika taasisi za
Serikali ikiwemo Hospitali, Polisi, Mahakama na Shule hapa nchini.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na
wananchi wa Turiani kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa Darajala Diwale.
Muonekano wa Daraja la Diwale linalounganisha wilaya ya Mvomero na Kilindi.
Mafundi wanaotengeneza vichwa vya treni katika karakana kuu ya TRL, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi Sanayejenga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akizungumza na
Wafanyakazi wa TRL (Hawapo pichani), Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Ucukuzi na Mawasiliano Eng.Wdwin Ngonyani, akifuatiwa na Kaimu
Meneja wa TRL Morogoro Eng.Yusto Goima na Meneja TANROADS Morogoro
Eng.Dorothy Mtenga.
Wafanyakazi
wa karakana kuu ya Reli Mkoani Morogoro wakimsiliza Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa (Hayupo pichani),
akiwapa muongozo wa kufanya kazi.
Post a Comment