Wanachama wa
Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza,
wameonya juu ya baadhi ya Wawekezaji nchini wanaotumia Vitega uchumi vya chama
hicho bila kufuata mikataba wanayopewa.
Wanachama hao walitoa kauli hiyo wiki hii baada ya Wawekezaji
wanaotumia majengo ya CCM Kata ya Kirumba, kudaiwa kukiuka masharti yao na
hivyo kutumia majengo hayo bila kuyalipia kodi ya pango kwa muda mrefu.
Ni kutokana na hatua hiyo, Wanachama hao walichukua maamuzi ya
kufunga Majengo hayo ambayo yanatumiwa na Tasisi ya Mikopo ya Wadoki pamoja na
Hotel ya Kirumba Resort, huku taratibu nyingine za kisheria zikiendelea, lengo
likiwa ni kuhakikisha kwamba watumiaji wa majengo hayo wanayalipia kodivwanayodaiwa
vinginevyo watafurushwa nje ya majengo hayo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Abubakary Francis
Kweyamba alithibitisha kwamba wanachama hao wamefikia maamuzi hayo, kutokana na
kutumia majengo ya chama katika kata hiyo huku wakiwa hawayalipii kodi na hivyo
kukisababishia chama usumbufu mkubwa wa kuendesha shughuli zake za kiofisi huku
akisisitiza msimamo wa kuendelea kuyafunga majengo hayo.
Katibu
Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya
ya Ilemela Acheni Maulidi, walisema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na wanachama
hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi
ngazi ya Mkoa ya Chama hicho na kuonekana kwamba wawekezaji hao hawatii
makubaliano yaliyofikiwa.
Suala
hilo lilifikishwa katika Kituo cha Polisi Kirumba na kila upande umetakiwa
kuwasilisha vielelezo vyake ili kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa
upangaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Meneja
wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba
mzungumzaji ni Mkurugenzi wake ambae alisema amesafiri huku Uongozi wa Wadoki
Saccos ukishindwa kupatikana.
Bonyeza HAPA KUTAZAMA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Post a Comment