Msanii wa
Muziki wa Bongo Fleva, ambaye pia ni Balozi wa Kampeni ya Amsha Mama
2016 Tundaman (kulia), akiongea jambo na mama Rishe Sophia Amri au
maarufu kwa jina la Mama Dayna muda mfupi baada ya kumkabidhi kiasi cha
shilingi laki moja ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza kampeni ya Amsha
Mama 2016, aliyoanza kutekeleza majuku yake mapema leo katika soko la
Tandale jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia zoezi hilo kushoto kwake ni
Mkurugenzi wa kampeni hiyo Joe Kariuki.
Balozi
wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundaman akichagua nguo moja wapo
zilizokuwa zikiuzwa na Mjasiliamali Sakina Thomas, kulia ni Mkurugenzi
wa Kampeni hiyo Joe Kariuki.
BALOZI wa
Kampeni ya Amsha Mama Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, ameanza rasmi
kutekeleza majukumu yake ya Kibalozi kwa kutembelea maeneo ya Tandale
jijini Dar es Salaam, ambapo amekukutana na baadhi ya kinamama
wanaojishughulisha na biashara ndogondogo.
Msanii
huyo ambaye amepewa Ubalozi huo kupitia waandaaji wa tamasha la AFWAB
AMSHA MAMA 2016, lililo chini ya Mkurugenzi mtendaji wa lebo ya Candy
na Candy Records Joe Kariuki, linalotarajiwa kufanyika Machi 25-27
mwaka huu katika uwanja wa Kedong ranch uliopo jiji la Naivasha nchini
Kenya.
Katika
ziara hiyo ya kushtukiza iliyofanywa na Tundaman pamoja na Muandaaji wa
Tamasha hilo Kariuki waliweza kutumia muda huo kuongea na baadhi ya
akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani
mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba katika soko hilo.
Tundaman
na Kariuki waliwapatia akina mama hao kila mmoja kiasi cha shilingi
laki moja ikiwa ni njia moja wapo ya kutimiza adhima yao ya kuwaamsha
akina mama wa Tanzania.
Kariuki
alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha akina mama katika tamasha
litakalowakutanisha na akinamama wengine kutoka nchi mbalimbali Afrika
kwa lengo la kujifunza na kupewa utaalam na jinsi kukuza biashara zao.
Post a Comment