Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya viongozi wa
vilabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na
upangaji wa matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa
katika ligi za ngazi mbalimbali za nchini
.
TFF imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi Kuu (VPL), Daraja
la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports Federation Cup
(ASFC) inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo
wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa.
Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia
kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au
mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali
zitachukuliwa .
TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi
kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo
ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini.
Post a Comment