Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Nachukua
Nafasi hii Kumpongeza Rais wa Awamu ya Tano John Pombe Magufuli kwa waraka wake wa elimu bure ambayo itagharamiwa
kwa fedha za walipa kodi ,ubunifu ambao unaweza kuwasaidia watoto wa Watanzania
ambao ni masikini wenye kipato cha chini.
Katika kipindi hiki Taifa limetoka katika Agenda ya kujadili
ubora wa elimu inayotolewa nchini,mitaala na mambo mbalimbali sasa mjadala mkubwa umeamia kwenye elimu bure.
Swali langu
ni kwamba elimu bure itakua na ubora ?,maana kwa sasa suala linalotiliwa mkazo
na kusimamiwa kwa nguvu zote ni elimu bure na sio elimu bora.
Wasi wasi
wangu ni kwamba taifa linaweza kuendelea kuteseka kwenye mitaala mibovu ,vitabu
ambavyo havikidhi huku viongozi wa ngazi za juu hadi za chini wakiendelea
kusisitiza elimu bure.
Kama elimu
bure haitaleta elimu bora basi hakutakua na tija yoyote kwa watanzania
,madarasa yataendelea kuwa maghala ya kuhifadhia watoto ama sehemu ya watoto
kukua.
Bado madai
ya walimu yanapigwa danadana na serikali ,walimu wanafundisha shingo upande huku
wakiwaza stahiki zao na kuzidiwa na ugumu wa maisha licha ya ugumu wa kazi.
Japo
hatuombei mgomo kwasababu wanaoathirika ni watoto wa mama ntilie,wamachinga ,wabangaizaji wa mjini ambao ndio idadi kubwa
ya watanzania wenye kipato cha chini huku watoto wa matajiri wakisoma shule za senti senti St……………….
Changamoto
ni nyingi katika huu waraka wa elimu bure ambao umezua mkanganyiko mkubwa kwa
viongozi,wazazi,walimu na watoto kutokujua maeneo ambayo serikali inachangia na
maeneo ambayo wananchi wanapaswa kuchangia.
Bado kuna
shule hazina madawati wanafunzi wanakaa chini lakini ni wanufaika wa elimu bure
kwa sababu shule inapata ruzuku ya kila mwanafunzi na ile ya uendeshaji wa
shule (capitation grand).
Bado kuna
shule hazina matundu ya chooo lakini ni wanufaika wa elimu bure na watanzania wameshatangaziwa kuwa wasitoe
mchango wowote elimu ni bure.
Bado watoto
wanashinda njaa mashuleni na ni wanufaika
wa elimu bure ,wanawezaje kupata elimu huku wakiwa na njaa na wazazi wameambiwa wasitoe mchango wowote.
Waraka
mwingine unapaswa kutolewa kwa wazazi waweze kutambua wapi wanapaswa kuchangia
na wapi hawapaswi kuchangia kama serikali haina uwezo wa kuchukua jukumu zima
la elimu bure na sio nusu nusu wala robo.
Kwa mtazamo
wangu elimu bure itashusha kiwango cha elimu nchini hususan katika shule za
serikali kwa kuwa jambo hili ni zito na
si jepesi ni kama vile serikali ilikua haijajiandaa vizuri kubeba hili.
Nilizungumza
na Meneja mmoja wa shule binafsi akaniambia wazazi wanawafuatilia watoto wao
sana katika shule binafsi kwa sababu wanatoa fedha nyingi tofauti na shule
binafsi wazazi hawalipi fedha nyingi na
hawafuatilii watoto wao.
Siungi mkono
wazazi kuchangia lakini pia kama serikali inaonekana haipo tayari kwa hili ni
bora kurudi kwenye mfumo wa wazazi kuchangia tusing`ang`ane na elimu bure
ikawagharimu Watoto wa masikini Watanzania
japo namini Tanzania ina utajiri wa rasilimali za kutosha kutoa elimu
Bure bila mipaka kama Viongozi wakiamua.
Waswahili
husema Bure inagharama bure hii inaweza kuwagharimu watanzania na taifa hususan
kupanda na kushuka kwa chati ya elimu nchini.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika.
0765938008
Post a Comment