PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YA AWAMU YA TANO ELIMU BURE? ELIMU BORA?
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Nachukua Nafasi hii Kumpongeza Rais wa Awamu ya Tano John Pombe Magufuli   kwa waraka wake wa elimu bure...

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Nachukua Nafasi hii Kumpongeza Rais wa Awamu ya Tano John Pombe Magufuli  kwa waraka wake wa elimu bure ambayo itagharamiwa kwa fedha za walipa kodi ,ubunifu ambao unaweza kuwasaidia watoto wa Watanzania ambao ni masikini wenye kipato cha chini.

Katika  kipindi hiki Taifa limetoka katika Agenda ya kujadili ubora wa elimu inayotolewa nchini,mitaala na mambo mbalimbali sasa mjadala  mkubwa umeamia kwenye elimu bure.

Swali langu ni kwamba elimu bure itakua na ubora ?,maana kwa sasa suala linalotiliwa mkazo na kusimamiwa kwa nguvu zote ni elimu bure na sio elimu bora.

Wasi wasi wangu ni kwamba taifa linaweza kuendelea kuteseka kwenye mitaala mibovu ,vitabu ambavyo havikidhi huku viongozi wa ngazi za juu hadi za chini wakiendelea kusisitiza elimu bure.

Kama elimu bure haitaleta elimu bora basi hakutakua na tija yoyote kwa watanzania ,madarasa yataendelea kuwa maghala ya kuhifadhia watoto ama sehemu ya watoto kukua.

Bado madai ya walimu yanapigwa danadana na serikali ,walimu wanafundisha shingo upande huku wakiwaza stahiki zao na kuzidiwa na ugumu wa maisha licha ya ugumu wa kazi.

Japo hatuombei mgomo kwasababu wanaoathirika ni watoto wa mama ntilie,wamachinga  ,wabangaizaji wa mjini ambao ndio idadi kubwa ya watanzania wenye kipato cha chini huku watoto wa matajiri wakisoma shule za  senti senti St……………….

Changamoto ni nyingi katika huu waraka wa elimu bure ambao umezua mkanganyiko mkubwa kwa viongozi,wazazi,walimu na watoto kutokujua maeneo ambayo serikali inachangia na maeneo ambayo wananchi wanapaswa kuchangia.

Bado kuna shule hazina madawati wanafunzi wanakaa chini lakini ni wanufaika wa elimu bure kwa sababu shule inapata ruzuku ya kila mwanafunzi na ile ya uendeshaji wa shule (capitation grand).

Bado kuna shule hazina matundu ya chooo lakini ni wanufaika wa elimu bure  na watanzania wameshatangaziwa kuwa wasitoe mchango wowote elimu ni bure.

Bado watoto wanashinda njaa mashuleni  na ni wanufaika wa elimu bure ,wanawezaje kupata elimu huku wakiwa na njaa  na wazazi wameambiwa wasitoe mchango wowote.

Waraka mwingine unapaswa kutolewa kwa wazazi waweze kutambua wapi wanapaswa kuchangia na wapi hawapaswi kuchangia kama serikali haina uwezo wa kuchukua jukumu zima la elimu bure na sio nusu nusu wala robo.

Kwa mtazamo wangu elimu bure itashusha kiwango cha elimu nchini hususan katika shule za serikali kwa kuwa jambo hili ni  zito na si jepesi ni kama vile serikali ilikua haijajiandaa vizuri kubeba hili.

Nilizungumza na Meneja mmoja wa shule binafsi akaniambia wazazi wanawafuatilia watoto wao sana katika shule binafsi kwa sababu wanatoa fedha nyingi tofauti na shule binafsi  wazazi hawalipi fedha nyingi na hawafuatilii watoto wao.

Siungi mkono wazazi kuchangia lakini pia kama serikali inaonekana haipo tayari kwa hili ni bora kurudi kwenye mfumo wa wazazi kuchangia tusing`ang`ane na elimu bure ikawagharimu Watoto wa masikini Watanzania  japo namini Tanzania ina utajiri wa rasilimali za kutosha kutoa elimu Bure bila mipaka kama Viongozi wakiamua.

Waswahili husema Bure inagharama bure hii inaweza kuwagharimu watanzania na taifa hususan kupanda na kushuka kwa chati ya elimu nchini.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika.

0765938008


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top