Gari
STK 9442 alilokua akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam mke wa
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda likiwa limeharibika
vibaya baada ya kupata ajali hii leo jioni eneo la Mkundi mkoani
Morogoro.
Mke
wa waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda amenusurika kifo
baada ya gari alilokua akisafiria kugongana na pikipiki mkoani Morogoro
hii leo.
Mama
Pinda aliyekua akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam akitumia gari STK
9442 liligongana na pikipiki MC647 BBA na kupondika eneo la Mkundi
mkoani Morogoro majira ya saa 8 mchana hiyo jana.
Habari
kutoka eneo la tukio zinasema kua chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa
bodaboda aliyeingia barabarani bila tahadhari na kupelekea mama Pinda,
msaidizi wake na dereva kupata majeraha huku mwemda bodaboda huyo
akipoteza maisha.
Majeruhi
walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro ambapo walipatiwa matibabu
kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutenge ni miongoni mwa viongozi waliofika eneo la tukio na kuwatembelea majeruhi katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Post a Comment