PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Kimenuka...Wakili Awadh Ali Adai Uchaguzi wa Zanzibar Haupo Kisheria..Adai ZEC Inashurutisha Wasiasa na Wananchi Kushiriki Uchaguzi Batili
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Wakili Msomi Awadh Ali amesema kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar haupo kisheria. Wa...


Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Wakili Msomi Awadh Ali amesema kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar haupo kisheria. Wakili Awadh,akihojiwa na ITV,amesema kuwa Katiba na Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar haitambui uchaguzi wa marudio.

Wakili Awadh amesema kinachofanywa na ZEC ni kuwashurutisha wanasiasa na wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio hapo Machi 20. Wakili Awadh amesema kuwa washindi wa uchaguzi wa mwaka jana walishapewa vyeti vya ushindi na hivyo hawawezi kupokwa vyeti vyao.

Kuhusu pendekezo la kukimbilia mahakamani kupinga uchaguzi wa marudio,Wakili Awadh amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Katiba haziruhusu kupingwa au kuchunguza ZEC kimahakama.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top