Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya jinai (ICC) imetakiwa kushughulikia malalamiko ya Viongozi wan chi za Afrika wakihishutumu
mahakama hiyo kuwa kandamizi kwa nchi za Kiafrika ile hali makosa ya jinai
hutokea karibu kila pembe ya dunia.
Kufuatia
shutuma hizo Umoja wa nchi za Afrika (AU) umetoa msimamo wake wa kupinga
mahakama hiyo kuonekana kuegemea zaidi kwenye nchi za jangwa la Sahara jambo
ambalo linapingwa vikali na viongozi wengi.
Waziri wa
Katiba, Sheria na Haki ,Dr.Harisson
Mwakyembe akizungumza katika semina
iliyoandaliwa na mahakama hiyo ameitaka kufanyia kazi manung`uniko ya bara la
Afrika licha ya Tanzania kuunga mkono shughuli za mahakama hiyo lakini bado iko
kwenye msimamo wa nchi hizo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Chama cha Wanasheria Waafrika (PALU) Donald Deya , amesema kuwa mahakama ya ICC inapaswa
kujitazama upya na pia viongozi wa Afrika wajitazame pia kwani pande zote mbili
zinaonekana kuwa na makosa .
Msajili wa
Mahakama ya ICC Herman Von Hebel ameipongeza
Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kupigania amani katika nchi jirani hususani
Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari na kusisitiza kuwa mahakama hiyo
itaendelea kushirikiana vyema na Bara la Afrika katika kutimiza majukumu ya
kuleta amani,haki na usawa duniani.
Mahakama ya Kimataifa ya AICC
inaendelea na semina ya wiki nzima kwa wanasheria na viongozi mbalimbali juu ya
jinsi ya kutumia mahakama hiyo kutetea haki za binadamu na utawala bora.
Post a Comment