Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimlisha chakula Narsa Ramadhan (2) akiwa na mama yake Tatu Saleh (kushoto) wakati wa hafla ya chakula kilichondaliwa kwa watoto na wazee wanaoishi katika makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.(Imeandaliwa na Modewjiblog)
Licha ya kuvaa taji la ulimbwende, Miss Tanzania 1999, Hoyce Anderson Temu
amekuwa mfano wa kuigwa kwa walimbwende waliopita wa taji hilo nchini
kwa kujitoa kusaidia jamii ya Tanzania kwa kutumia nafasi aliyonayo
nchini.
Hoyce
ambaye ni mzaliwa wa Arusha amekuwa mstari wa mbele kusaidia Watanzania
ambao wanamatatizo mbalimbali kama ya kiafya na elimu ambapo amekuwa
akitoa misaada na muda mwingine kutafuta wadhamini ili kusaidia jamii
ambayo ameifikia kwa muda huo.
Baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania
ni pamoja na kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu
akiwepo mtoto Hamisi ambaye alimsaidia kwenda kupata matibabu ya mguu
wake.
Kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania
kinachorushwa upitia Channel Ten kila siku ya jumapili, saa 9:30 usiku,
Hoyce amefanikiwa kuandaa vipindi zaidi ya 1,000 maeneo mbalimbali
nchini na katika maeneo yote ambayo ametembelea amefanikiwa kutoa msaada
kulingana na mahitaji yanayohitajika.
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akisalimiana na mmoja wa wazee wenye ulemavu uliotokana na ugonjwa wa ukoma, Mganga Shija (66), wakati alipotembelea makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya shughuli ya kijamii kuuaga mwaka 2015 na kukaribisha mwaka mpya 2016.
Uamuzi wa Hoyce kuwa
na moyo wa aina hiyo ulikuja baada ya kutambua nafasi aliyonayo kwa
jamii na kuona wingi wa matatizo waliyonayo Watanzania wenzake na hivyo
kufikia uamuzi wa kuanzisha kipindi ambacho kwa sasa kina zaidi ya miaka
5 na bado ameonyesha nia ya dhati kuendeleza kipindi hicho.
Kwa kutambua huduma yake kwa jamii, Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliwahi kunukuliwa akimtaja Hoyce Temu kama
mlimbwende bora kuliko wote wakati alipotembelea kituo cha Nunge
kilichopo Kigamboni, Dar Es Salaam kinachotumika kutunza wazee
wasiojiweza na walemavu wasiokuwa na uwezo.
Pamoja ya kujitoa kusaidia
Watanzania wenzake walio na uhitaji na kutumia muda wake mwingi katika
huduma za kijamii, baadhi ya watu wasio na nia njema na Hoyce wamekuwa wakimwandika vibaya ilimradi tu kumchafulia jina katika jamii inayomzunguka.
Mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Hoyce Temu akirekodi moja ya kipindi chake cha Mimi na Tanzania na mtoto ambaye aliaga dunia kabla ya matibabu.
Kama Watanzania ambao tunapenda kuona huduma za kijamii zinaboreshwa kupitia kwa Hoyce Temu na kipindi chake cha Mimi na Tanzania tuna wajibu wa kuhakikisha tunaungana kwa pamoja kumsaidia Hoyce kama mwanamke shujaa na mwenye moyo wa huruma kuwasaidia Watanzania ili kufikia malengo ambayo ameweka kuisaidia jamii..
Muungano wa Watanzania ndiyo pekee utakaozidi kumfanya Hoyce kuwa
na moyo zaidi wa kusaidia Watanzania wenzake wenye uhitaji na amekuwa
mtu ambaye anaonekana kuzingatia maoni ambayo anapewa na Watanzania
wenye nia njema na yeye ili kuzidi kuwa mtu mwema katika jamii ya
Tanzania na dunia kwa ujumla.
Hata hivyo licha ya watu wachache
kumchafua amekuwa mtu ambaye hajishughulishi kuwajibu wenye nia mbaya na
mipango yake kuwasaidia Watanzania na muda mwingi kuendelea kuitumia
jamii na kufanya kazi kwenye kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano katika
ofisi za Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini.
Pia licha ya kazi anazofanya Hoyce kwa sasa anatumia muda wake mwingine kuongeza elimu yake kwa kuchukua PHD ya mambo ya Mawasiliano.
Post a Comment