Nimesoma nukuu inayosema kwamba binadamu siku zote tunapenda kupata sifa
isiyo stahili kwa mazuri tu lakini mabaya tunasingizia bahati mbaya.
We always take credit for the good and attribute the bad to fortune.
Maneno haya yamenichoma moyoni kwani nimeona kuwa yana ukweli katika
maisha yetu ya kila siku. Nimefanya kazi siku zote bila kujali mwenzangu
au wenzangu wanafanya nini, na sipendi kutangaza mafanikio yangu yote.
Ila kuna watu maishani ambao wamenisaidia kufika hapanilipo na hata wao
huwa wanaishi kwa kufuata msingi wa kuwa “tendawema uende zako”, na
hawajawahi kukaa na kujitangazia kuwa wao ndo wamenifikisha hapa nilipo
ingawa ni kweli.
Cha ajabu ni pale kuona kuwa kuna mtu ambaye namfahamu kawaida tu na
hatuna mazoea wala hajuiniishivyona nimefika vipi hapa nlipo
inasemekaana kuwa yeye ndo kanifikisha hapa nilipo. Kibaya zaidi si kuwa
kaongea hadharani na marafiki zake bali ni kuiweka bayana katika
gazeti.
Kitendo hiki kimenishtua na kunisikitisha kwanimimi binfasi sijawahi
kuongea katika magazeti kuhusu maisha ya mtuwala kudai kuwa mi ndo
nimemfikisha mahala fulani. Lakini chakusikitisha zaidi, watu ambao
kweli wamenisaidia katika maisha yanguhawajawahi kukaa na ‘kuuza sura’
kwa kutumia jina langu.
Mafanikio yangu madogo nilonayo sasa ndani na nje ya nchi yamefikiwa kwa
juhudi zangu na zawatu wachache, hii ni pamoja na kupatikana kwa
mkataba wangu wa nje(Afrika Kusini) na mkataba na maelewano yote ni kati
yangu mimi,kampuni yangu ya Afrika Kusini na kampuni yangu mama ya
CompassCommunications.
Hatua zozote zilizochukuliwa hazikumhusisha mtanzaniamwingine. Na hata
katika siku zijazo, itaendelea kuwa hivyo. Kwaheshima na taadhima naomba
mhusika na wahusika, waache kuongeleamaisha yangu, mafanikio yangu,
kwani haiwahusu.
Pia naomba wanajamii wenzangu mkisikia kitu kinazungumzwa ambacho
hakijatoka kwangu au kampuni yangu mama, basi wajue atakuwa ni binadamu
mwingine ambaye ametetereka na kuingia katika mtego ule wakutaka kupata
sifa asizostahili.
Mwisho kabisa napenda kuwashukuru wote ambao wapo sambamba na watanzania wote kwa ujumla
Regards,
Flaviana Matata
Post a Comment