Mkuu
wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo,
Obedi Laiser akielezea kuhusu gawio la mwaka huu kwa watumiaji wa Tigo
Pesa, kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha
|
Waandishi
wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu gawio la mwaka huu la
tigo pesa katika mkutano uliofanyika mapema leo katika makao makuu ya
Tigo Kijitonyama Dar es salaam.
|
Mkuu
wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo,
Obedi Laiser akijibu maswali ya waandishi wa habari (Hawapo pichani)
kuhusu gawio la mwaka huu kwa watumiaji wa Tigo Pesa, kushoto kwake ni
Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha
Dar es Salaam, Januari 13, 2016- Kampuni
inayongoza katika kuleta maisha ya kidijitali kwa jamii, Tigo,
imetangaza tena malipo ya robo mwaka ya shilingi bilioni 4.4 (dola
milioni 2.1) kwa watumiaji wake wa huduma ya Tigo Pesa wapatao milioni
4.6.
“Gawio
hili la faida linalipwa kwa watumiaji wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja
binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wetu wa kibiashara, kila
mmoja kutokana na thamani ya fedha aliyojiwekea katika akaunti yake ya
Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa
njia ya mtandao, Obedi Laiser.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Laiser
amesema kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza Tigo kuwalipa gawio la faida
watumiaji wa Tigo Pesa kwa mwaka wa 2016 akibainisha kuwa malipo hayo
ni faida inayopatikana kutokana na amana ya mfuko wa Tigo Pesa
uliyowekezwa katika benki za kibiashara hapa nchini.
“Tunayo
furaha kubwa kutangaza gawio hili la faida kwa mara ya saba mfululizo
tangu tulivyoanza kufanya hivi mwaka 2014. Bila shaka hii inaonyesha ni
jinsi gani Tigo inajizatiti kuwaletea watanzania maisha bora ya malipo
kwa njia ya mtandao,” amesema Laiser.
Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kutoa gawio kwa wateja wake mwaka 2014
“Tunaamini
gawio hili la kwanza la faida ya Tigo Pesa kwa mwaka 2016 litakuwa ni
kivutio kikubwa kwa mamilioni ya watumiaji wa Tigo Pesa katika
kufanikisha mahitaji yao mbalimbali ya kifedha ya mwanzo wa mwaka,”
amesema Laiser.
Malipo
haya kwa watumiaji wa Tigo Pesa hutolewa kwa mujibu wa mwongozo wa
Benki Kuu uliotolewa mnamo Februari mwaka 2014. Mpaka sasa Tigo imelipa
jumla ya 35.5bn/- kwa wateja wake tangu kuanzishwa kwa utaratibu huu
mwaka juzi na kampuni hiyo.
|
Post a Comment