Rais Magufuli akiwa anaongea na wananchi wa eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji la Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha
Msafara
wa Rais John pombe magufuli uliokuwa ukielekea monduli (jana)
umesimamishwa na wananchi katika eneo la Mbauda lililopo ndani ya jiji
la Arusha ili kushinikiza kuta kero zao
na changamoto zao ikiwemo kuwepo na
kiwanda cha mafuta ya kupikia
cha Mount Meru Mill kinachodaiwa kuchafua mazingira na kuatharisha
afnya za wakazi wa eneo hilo.
Wananchi hao ambao walijikusanya kuanzia mida ya saa mbili
kamili asubui mbali na kumueleza rais huyo kero zao pia walitumia nafasi hiyo
kumpongeza kwa kazi anayofanya na kumuomba aendelee kutumbua majipu
yaliyopo humu nchini.
Akiongea
mbele ya rais mara baada ya kupewa nafasi mmoja wa wanachi wa eneo
hilo la mbauda Dhabiti Abubakari alimuomba rais awasaidie
kutatua tatizo la kiwanda hilo kutiririsha maji machafu ya kiwandani
kwani tatizo hilo ni baya na linawaaribia
mazingira na kuatarisha afya zao .
‘’musheshimiwa rais tunapenda utusaidie apa kwetu mbauda
tuna kero kubwa inatusumbua kunahiki kiwanda cha mafuta ya kupikia cha mount
meru mill kimekuwa kinatiririsha maji machafu ya kiwandani huku nje ambapo
wananchi wanaishi , kiwanda hichi hakijajenga mitaro ya kupitisha maji machafu hivyo maji yote
machafu yakitoka huko kiwandani yanaingia huku majumbani kwetu hivyo
muheshimiwa tunaomba utusaidie hili tatizo kwani kiwanda hiki kipo ndani ya
makazi ya watu sasa inatuatarishia afya zetu pamoja na za watoto wetu ambao
wanacheza uku mitaani pia tunaweza kupata magonjwa ya milipuko kama
kipindupindu maana maji haya ni machafu sana”alisema Dhabiti
Akijibu swala hilo Rais magufuli alisema kuwa amelisikia na aliwaagiza
mamlaka ya usafi wa mazingira nemc kulifuatilia swala hili mara moja .
Aidha magufuli alitumia muda huo kuwashukuru wananchi wa
jiji la Arusha kwa jinsi walivyoendelea kujitokieza kumpokea na kuwahaidi
ataendelea kutekeleza yale yote aliyoyahaidi katika kipindi alipokuwa akifanya
kampeni.
Alisema kuwa kipindi hiki akuja arusha kwa ajili ya kuongea
na wananchi hivyo basi ataandaa siku na kuja rasmi arusha kufanya mkutano
mkubwa ambao pia atatumia mda huo kusikiliza kero za wananchi wa jiji la hilo.
Post a Comment