NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Uongozi wa
Timu ya Panone Fc ya Mkoani Kilimanjaro inayoshiriki Ligi daraja la kwanza
Tanzania Bara (FDL), umesema kuwa haukubaliana ni maamuzi yalitolewa na kamati
ya Uendeshaji na usimamizi wa ligi kwa Kuwapiga faini ya sh 1,000,000.
Panone
wamekumbwa na rungu hilo baada ya timu hiyo kugombea kuingia mlango wa VIP
katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
Mkoani Tabora walipokuwa wakicheza dhidi ya Timu ya Polis Tabora januari
2 Mwaka huu.
Msemaji wa timu
hiyo Cassim Mwinyi Amesema kuwa maamuzi hayo sio ya kweli kutokana na wao
kukuta geti la kuingilia kufungwa kisha kuwaona wenyeji wao Timu ya Polis
Tabora wakiingilia Mlango mwingine ndipo nao wakawafuata na kukutana na kizuizi
cha Polis waliokuwa wakilinda mlangoni hapo.
“Tulitoa
taarifa kwa kamishna wa mchezo huo Shabani Funyaro na hakuweza kutusikiliza
ndipo tukaona tusonge mbele kwa kuiandikia TFF malalamiko yetu juu ya mchezo
huo”
“Maamuzi
haya yanaukakasi, utawezaje kumfungia kamishna wa mchezo kwa ripoti yake mbovu
halafu unatoa maauzi kwa ripoti mbovu, sasa hapo tunashindwa kuelewa juu ya
maamuzi nwaliyoyachukua hadi tukapigwa faini hiyo” alisema Mwinyi
Hata hivyo
timu hiyo imeamu kuchukua maamuzi ya juu kwa kuandika barua wakikata rufaa kwa
TFF juu ya timu ya Polis Kuwachezesha wachezaji wawili kinyume na taratibu na
kanuni za soka letu kwa kuwachezesha wachezaji raia wa Nigeria na mwingine
kutoka Uganda bila kufuata taratibu.
Kesho Jumamosi Panone wataikaribisha timu ya Geita Gold
Star mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Ushirika katika mwendelezo wa ligi
daraja la kwanza, timu ya Geita Gold Star inayoongoza ligi hiyo katika kundi
lao ikiwa na pointi 21 ikifuatiwa na JKT Oljoro yenye Pointi 19.
Post a Comment