ARUSHA.
Timu ya AFC
inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania Bara (SDL), imejikuta ikilazimishwa
suluhu na timu ya Hai SC inayoshiriki Ligi ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro
katika mchezo wa Kirafiki uliochezwa mwanzoni mwa wiki Katika uwanja wa Seikh
Amri Abeid Mkoani hapa.
Timu ya AFC
ilicheza kwa umakini Mkubwa katika mchezo huo, huku ikishindwa kufunga mabao ya
wazi kutokana na ukuta wa Timu ya Hai waliouweka ili kuhakikisha hawaruhusu
bao.
AFC inatarajia
kucheza mchezo mwingine wa Kirafiki kabla ya kipute cha ligi daraja la pili
kuanza kutimua vumbi Januari 23, huku AFC ikianza kucheza na timu ya Pamba
januaru 24 katika uwanja wake wa Nyumbani wa Seikh Amri Abeid.
Hata hiyo ratiba
ya mchezo huo inaonekana kuingiliana kutokana na siku ambayo Pamba inatakiwa
kucheza na AFC hapa Arusha ndiyo siku pia timu ya Pamba itatakiwa kucheza na
Toto African katika mchezo wa FA Huko Mwanza.
Katibu msaidizi
wa Timu ya AFC Charles Mwaimu Alisema kuwa hawajui nini kitatokea juu ya
kuingiliana kwa ratiba hiyo huku wao wakisubili tamko kutoka ngazi husika.
“Hatujapokea
maelezo yoyote kutoka TFF juu ya mwingiliano wa ratiba hiyo, sisi tunasubili
tuone itakuwaje na tupo kwa tayari kwa mabadiliko yoyote yatakayojitokeza”
Alisema Mwaimu.
Mpaka sasa AFC
inaalama moja tu katika Ligi hiyo baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya
ndugu za Timu ya Madini FC mchezo uliokuwa wa kufunga mzunguko wa kwanza katika
uwanja wa Seikh Amri Abeid
Post a Comment