Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo
mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha
wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
|
Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Tigo kwa mbio za Nusu Marathon mbio
hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha
wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
|
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga(watatu kushoto, ).akizindua mbio za
Kilimanjaro Marathon kwa upande wa Moshi. Wengine ni wadhamini wakuu wa
mbio hizo kutoka kushoto, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry
Kinabo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania-Kilimanjaro na Tanga,
Richard Temba, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro,
Listone Metacha na Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Caroline
Kakwezi.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
|
Wageni
waalikwa ambao ni wadhamini wa Kili Marathon wakifurahia jambo baada
ya Mkuu wa wilaya Mh Novatus Makunga kuzindua mbio za Kili Marathon kwa
upande wa Moshi ambapo zitafanyika hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
|
Mbio za Nusu Marathon 2016 zimezinduliwa jana mjini Moshi, huku ikiwa imebaki mwezi moja kabla za mbio hizo kufanyika.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari alisema
mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha
wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.
“Tumeonelea ni vizuri kuzindua mbio hizi rasmi hapa Moshi ambako zitafanyika ili kuashiria kuwa mambo yamekamilika,” alisema.
“Tigo
imeingia mwaka wake wa 2 kama mdhamini wa mbio za kilomita 21.2 hizi.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, wadhamini wengine wa mashindano hayo ni
Kilimanjaro beer 45, Gapco kwa km 10 viti vya magurudumu na baiskeli ya
kunyonga kwa mkono na Grand Malt kwa km 5.
Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair na Keys Hotel.
Alisema
Tigo imewekeza zaidi ya Sh Millioni 200 katika mashindano hayo na kuwa
hapo badaye watatangazo mchanganuo mzima wa zawadi zitakazotolewa.
Alitoa
shukrani za pekee kwa mkoa wa Kilimanjaro na chuo kikuu cha Ushirika
MOshi (MoCu), zamani kikiitwa MUCCoBS kwa kuwa wenyeji wa mashindano
hayo.
Akizindua
mbio hizo mjini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makung,
aliwapongeza Kilimanjaro Premium Larger,Tigo wadhamini wengine na
wandaaji kwa kujielekeza vyema kila mwaka, akiongeza kuwa
mashindanoyametokea kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kimichezo
ndani na nje ya nchi.
“Mashindano
haya pia yamekwenda mbali zaidi katika kukuza utalii, kwani wanariadha
wa kimataifa na wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hiyo
kufaidisha uchumi wan chi,” alisema Makunga.
Makunga
aliawataka wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanajiandaa vyema ili
watwae zawadi nyingi zaidi kwa kadiri zilivyopangwa kwa kila mbio.
Aliongeza kwamba wizara yake inaunga mkono kabisa ubunifu kama huo na
kuzitaka kampuni nyingine kufuata nyayo hizo kwa kudhamini mashindano
hayo kila mwaka.
Aliwapongeza
wandaaji, Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa Executive Solutions,
Chama cha Riadha Tanzania (RT) na wizara yenye dhamana ya michezo kwa
kuhakikisha siku zote kwamba tukio hili linafikiwa .
“Mbio
hizi zimeleta mwamko mpya katika riadha hapa nchini kwa kuwapa fursa
vijana wetu wanaochipukia kuweza kujipima na wanariadha mashuhuri
kimataifa. Changamoto hii imekuwa na faida kubwa,ambapo vijana wetu
wameweza kutambua uwezo wao na kuweza kujiamini zaidi wanapokwenda
kushiriki mashindano mbalimabli kwenye nchi za kigeni,” alisema.
Meneja
wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, alisema kwamba kampuni yake
imefurahishwa kupata fursa ya kudhamini mbio za nusu marathoni kwa
kilimota 21 kwa mwaka wa pili mfululizo.
“Natoa rai kwa washiriki wajiandae vizuri ili safari hiituweze kunyakua mataji mengi,” alisema Kinabo.
Meneja
Masoko wa Gapco Tanzania, Caroline Kakwezi, ambaye kampuni yake
inadhamini mbio za kilomita 10 kwa wanaotumia viti vya magurudumu na
wale wanaonyonga baiskeli kwa mikono ambazo wanazidhamini, alisema
zimekua na mvuto mkubwa na ushindani mkubwa pia na kwamba katika mwaka
wao wa tano katika udhamini wameshuhudia mbio hizo zikikua.
“Tunawashukuru
wateja wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono, safari hii tutatoa
usafiri, malazi na chakura kwa washiriki wote kutoka Dar es Salaam
katika mbio hizi za walemavu na yote haya hayawezekani bila ushirikiano
tunaoupata kutoka kwa wateja wetu”alisema.
Post a Comment