PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Serikali kufufua vyuo vya Ufundi vya watu wenye ulemavu
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mwalimu wa watoto wenye uoni hafifu Bi. Kulwa Andrea akielezea changamoto ya uhaba wa vitabu vya Nukta Nundu kwa Naibu Waziri (Watu wen...
Mwalimu wa watoto wenye uoni hafifu Bi. Kulwa Andrea akielezea changamoto ya uhaba wa vitabu vya Nukta Nundu kwa Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipotembelea shule ya Irente Wilayani Lushoto Januari 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza umuhimu wa kuwapa kipaumbele cha elimu watu wenye ulemavu, alipotembelea shule ya Irente Wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, Januari 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwalimu Adam Sheah wa Shule ya Irente Lushoto akitoa neno la ufunguzo wa kikao cha Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe.Dkt. Abdallah Possi na wafanyakazi wa shule hiyo, alipofanya ziara shuleni hapo Januari 5,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na. Mwaandishi Maalum
Serikali imedhamiria kufufua vyuo vya ufundi vya watu wenye ulemavu nchini ili kuendana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kutatua changamoto na kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu hapa nchini.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Watoto wenye Ulemavu wa Viungo cha YDPC Tanga wakati wa ziara yake ya kwanza Mkoani Tanga Januari 4, 2016.

Mhe.Possi alieleza kuwa,”Serikali itafanya jitihada zote kuhakikisha vyuo vilivyofugwa na vinavyoendelea na ufundishaji vinaboreshwa na kurejeshwa katika hali nzuri”.
Waziri Possi alisikitishwa na hatua za kufungwa kwa baadhi ya vyuo kama Chuo cha Ufundi cha watu wenye ulemavu cha Misiwani na aliahidi ifikapo Juni, 2016 chuo hicho kiwe kimeboreshwa na kufunguliwa ili kufikia malengo yaliyokuwepo awali. “kufungwa kwa baadhi ya vituo na vyuo vya ufundi vya watu wenye ulemavu ni changamoto kwa serikali kwani inaongeza utegemezi na uhitaji wa watu wenye makundi maalum”alisema Mhe. Possi.
Wakati wa ziara hiyo mkoani Mhe. Possi alifanikiwa kutembelea maeneo ya Makazi ya Watu wenye ugonjwa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top