Title: NMB na Kampuni ya John Deere Kutoa Mikopo Rahisi kwa Wakulima
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5
Des:
...
Na Mwandishi Wetu BENKI ya NMB kwa kushirikiana na Kampuni maarufu kwa
uuzaji wa matrekta ya John Deere zimeingia makubaliano ili kufanikisha
kuwakopesha matrekta wakulia wanaochipuki kwa lengo la kuwawezesha
waendelee kufanya vizuri kwenye kilimo cha kisasa.
Katika makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Banki ya
NMB imekubali kutoa mkopo ambao utamuwezesha mkulima kununua trekta hilo
huku akiurejesha taratibu, Hata hivyo Kampuni ya John Deere itatoa
mafunzo ya kilimo cha biashara kwa mkulima aliyenufaika na mkopo huo
pamoja na kumfundisha matumizi bora ya kifaa hicho cha kilimo.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano hayo, Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alisema
benki yao inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo na inavyochangia kukuza
uchumi wa Tanzania hivyo kuamua kuwawezesha wakulima ili kuchochea
ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
“…Upatikanaji wa mikopo kwa wakulima siku za nyuma ulikuwa ni kikwazo
kikubwa katika maendeleo ya kilimo…hivyo makubaliano haya yanakuja
kuleta suluhisho kwa wakulima hasa katika eneo la kupata vifaa muhimu
vya kilimo cha kisasa kama matrekta yanayoendana na mabadiliko ya
teknolojia,” alisema Mponzi.
Alisema kwa kutambua mchango wa sekta ya kilimo tayari Benki ya NMB
imewasaidia wakulima wadogo zaini ya 600,000 kupata mitaji ya mikopo kwa
ajili ya uzalishaji wa mazao anuai ya kilimo pamoja na kuendesha
mafunzo ya kijasiliamali kuwajengea uwezo makundi yote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya John Deere, nchi za Afrika
Kusini mwa Jangwa la Sahara, Antois van der Westhuizen alisema mikopo
hiyo inayotolewa kwa wakulima inalengo la kuwainua wakulima wadogo ili
waweze kubadili kilimo chao kuwa kilimo endelevu kinachotumia vifaa vya
kisasa yakiwemo matrekta ya kilimo, kuvunia na kusafirisha mazao kutoka
shambani hadi eneo linalokusudiwa.
“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo katika nchi za Afrika, John
Deere kwa kushirikiana na NMB tunategemea kuweka mifumo itakayowawezesha
wakulima wadogo ili kuleta ufanisi katika shughuli nzima ya kilimo.
Ufanisi katika manunuzi ya pembejeo, uzalishaji na pia matumizi ya
teknolojia za kisasa (mbegu, mbolea na hata vitendea kazi-mashine) na
hata ufanisi katika kutafuta masoko ya mazao yao mojakwa moja,” alisema
Westhuizen.
Post a Comment