NA,
YOHANA CHALLE.
ARUSHA
Timu ya Panone FC
imefanikiwa kupata pionti tatu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzunguko wa
pili wa ligi daraja la kwanza (FDL), baada ya kuifunga JKT Kanebwa 2-0 katika
uwanja wa ushirika Mkoani Kilimanjaro.
Ushindi huo
umekuwa wa kwanza kwa kocha mkuu wa timu hiyo Felx Minziro tangu atue katika
timu hiyo ya matajiri wa Mafuta baada ya kufungwa michezo yote miwili iliyopita
dhidi ya JKT Oljoro 2-1 na Polisi Tabora 2-1.
Mabao yote ya
Panone fc yamefungwa na Ally Mseje bao la kwanza akifunga dakika ya 65
kwa mkwaju wa penati na lile la pili akifunga dakika ya 84.
Mara baada ya
mchezo huo kocha mkuu wa Panone Felix Minziro alisema kuwa sasa ligi ndio
imeanza kwake kutokana na kukizoea kikosi chake kilichokuwa kimechanganyika
wachezaji wengi wa zamani na wale walioingia katika dirisha dogo la usajili.
Panone watakuwa
na kibarua kigumu katika mchezo unaofuata watakapoikaribisha Geita Gold Star
kutoka Mkoani Geita timu ambayo inapigania kupanda ligi kuu wakiwa wanapishana
kileleni na JKT Oljoro.
Kwa upande wa
Oljoro wamezidi kuambulia sare baada ya kubanwa na Rhino nyumbani ya bao 1-1
kisha juzi Jumamosi kushikwa ugenini dhidi ya Polis Mara ya bao 1-1 na
kufikisha pointi 19
Post a Comment