Picha mbalimbali zikimuonesha Mbunge wa Monduli Julius Kalanga (kulia) akiangalia Bweni la Shule ya
Sekondari ya Edward Lowasa lilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia
jana.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Bweni la
wanafunzi katika shule
ya sekondari ya Edward Lowasa iliyopo
wilayani Monduli mkoani Arusha limeteketea kwa
moto na wanafunzi
zaidi ya 70 wa kidato cha kwanza
wamelazimika kupewa likizo ya
wiki moja baada
ya vitu vyao kuteketezwa na moto
ikiwemo magodoro,nguo pamoja na vitabu .
Mwalimu mkuu
wa shule hiyo
Salum Selemani alisema moto
huo ambao umetekeza mali
zote za wanafunzi
na majengo unaodaiwa
kusababishwa na hitilafu
ya umeme za ulianza
saa nne usiku
wakati wanafunzi wakiwa
darasani wanajisomea na
hakuna aliyejeruhiwa japo baadhi
yao walikumbwa na hofu
iliyosababisha wapoteze fahamu na
kukimbizwa hosipitali .
Salum
amesema kuwa kwa sasa chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme
ingawa bado uchunguzi zaidi haujafanyika kubaini chanzo cha moto huo licha ya
kujiridhisha kuwa wanafunzi wanapokua shuleni hapo hawatumii simu wala chombo
chochote cha moto kwa maana ya kiberiti au mshumaa.
Mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na
usalama ya wilaya ya monduli
ambaye pia ni
Mkuu wa Wilaya
Bwana Francis Miti Alisema wanafunzi
wote wako salama
na wamefikia hatua ya
kuwapa likizo fupi ili
waweze kutulia wakati
jitihada kuwawezesha kuendelea
na masomo zikifanyika .
Mwenyekiti
wa Halmshauri ya Wilaya ya
Monduli Issack Joseph
na Mbunge wa jimbo la Monduli
Bwana Julius Kalanga alisema kuwa kwa sasa wako kwenye mpango wa
kuhakikisha kuwa wanatafuta magodoro na mahitaji muhimu ya kujenga bweni hilo
ili wanafunzi waweze kurejea masomoni.
Kalanga
amesema kuwa kumekua na matukio ya kujirudia rudia ya shule kuungua moto hivyo
walimu ,wazazi na wanafunzi wanapaswa kukaa pamoja na kujadili namna ya
kudhibiti matatizo yanayosababisha moto huo pamoja na kuhakikisha kuwa vyombo
vya kudhibiti moto (fire extinguisher) vinafungwa kwenye kila jengo la
serikali.
Alisema juhudi
za serikali,mashirika na watu binafsi zinahitajika kuhakikisha kuwa bweni jipya
linajengwa na wanafunzi wanarejea katika masomo licha ya kuunguliwa na vifaa
mbalimbali ikiwemo vitabu,nguo ,magodoro pamoja na masanduku.
|
Post a Comment