Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya piwa zilizokutwa
kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini Arusha katika
operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe
hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji,Picha na
Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wananchi wa
Mtaa wa Matejo uliopo jijini Arusha wameiomba serikali iwapatie mikopo ili
waweze kufanya shughuli mbadala za kujiingizia kipato badala kujishughulisha na
uuzaji wa pombe haramu ambazo zinadaiwa kuwa sababu mojawapo ya kuenea kwa
ugonjwa wa kipindu pindu kutokana na mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji
wake.
Wananchi hao
wakizungumza katika operesheni ya tokomeza
kipindupindu iliyoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ,kwa kushirikiana na
Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama wameteketeza mitambo ya kupikia
pombe hizo aina ya piwa,dadi na chang`aa ambazo pia huathiri afya za watu.
Ester
Stephano Shaka ambaye ni Muuzaji wa
pombe hizo na Wilfred Lyakimu na walisema kuwa maisha yao yanategemea biashara
ya pombe za kienyeji ambazo huwasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji ya
nyumbani hivyo ameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya biashara
mbadala badala ya kutumia nguvu kutokomeza biashara hiyo.
“Tunategemea
shughuli ya kupika na kuuza pombe za kienyeji kuendesha maisha yetu ,serikali
haiwezi kuwaajiri watu wote tunaiomba serikali itutafutie shughuli mbadala
kwani hapa ndio tunapata chakula na mahitaji muhimu “ Alisema Wilfred
Mkazi wa Matejo
Jovan George alisema kuwa kutokana na tatizo la ajira limewapelekea watu wengi
kujiingiza katika biashara hiyo na matumizi ya pombe hivyo ameitaka serikali
kutafuta njia mbadala .
Mkuu wa
Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha ,James Lobikoki alisema kuwa uteketezaji wa
pombe haramu ni moja kati ya jitihada wanazozifanya katika utekelezaji wa operesheni tokomeza kwani
kutokana na mazingira machafu ya uandaaji wa pombe hizo kwani zoezi hilo ni
endelevu.
Alisema Ugonjwa
wa kipindupindu umeenea katika maeneo mengi nchini tayari wananchi wameanza
kuchukua tahadhari ya kuweka mazingira safi licha ya baadhi ya maeneo
kukithiri kwa uchafu hivyo kukwamisha
jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.
|
Post a Comment