Na Krantz Mwantepele.
Tanzania
ya leo, imepitia mabadiliko mengi yanayogusa kila sekta tangu
ilipojikomboa na kuwa nchi huru baada miaka 53 ya utawala wa kikoloni.
Kwa
mfano, katika kipindi hicho hadi sasa, nchi imeshuhudia kuimarika kwa
huduma mbalimbali za kijamii. Kwa uchache, huduma hizi ni pamoja na
afya, elimu, demokrasia, utalii, viwanda na miundombinu mbalimbali.
Katika
sekta ya elimu, ongezeko kubwa la shule kuanzia ngazi ya awali hadi
chuo kikuu limeshuhudiwa. Hii ni moja ya hatua kubwa kuwahi kufikiwa
tangu nchi ilipoanza kujitawala. Katika sekta ya afya, hospitali,
zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa wingi kutegeme mahitaji ya
watu.
Miundombinu
ya barabara imeimarika maradufu na kuifanya Tanzania kuongoza Afrika
Mashariki kuwa na barabara zenye lami kwa kilomita nyingi. Lakini pamoja
na mafanikio hayo, nchi imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali
katika kila hatua ya kujaribu kuboresha huduma na mahitaji ya kijamii.
Miongoni
mwa changamoto hizo ni usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na
ubora wa huduma zinazotolewa. Viwango vya ubora kwa huduma zinazotolewa,
vimekuwa vikipungua kadri siku zinavyokwenda na sababu kubwa ni udhaifu
wa usimamizi kutoka kwa mamlaka husika.
Udhaifu
huu umesababisha wananchi ambao kimsingi ndiyo walipa kodi za serikali
kulalamika kila siku. Ikumbukwe kuwa ukusanyaji mzuri wa kodi na kuweka
matumizi wazi husaidia kuboresha huduma mbalimbali ndani ya jamii.
Ili
kuepukana na utawala mbovu usiojali wala kuheshimu misingi ya utawala
bora, kuna haja ya wananchi kufanya kazi pamoja. Hapa ndipo tunapouona
mpango wa Chukua Hatua kama mkombozi kupita uraghbishi, yaani kuwahuisha
na kuwahamasisha watu walionyimwa haki kujiona kama watendaji wakuu na
siyo kama watu wa chini mbele ya matabaka mengine.
Ni
sahihi, kuona wananchi wakisimama imara, kujithamini na kujenga uelewa
wa misingi ya uchambuzi wa hali ya maisha yao. Lakini pia, kuwawezesha
watu kuwa na utamaduni wa kuthubutu kujaribu mambo mbalimbali ya
maendeleo. Watu hao tunawaita waraghbishi.
Waraghbishi
hawa wameanza uraghbishi tangu mwaka 2010 pale mpango wa Chukua Hatua
ulipoanza katika wilaya za Bukombe, Kahama, Shinyanga Vijijini, Maswa,
Kishapu na Bariadi.
Ziliongezeka
wilaya mbili, Itilima na Mbogwe baada ya baadhi ya wilaya za Mkoa wa
Shinyanga kuhamishiwa mikoa mipya ya Geita na Simiyu na wilaya ya
Ngorongoro kwa mkoa wa Arusha.
Uraghbishi
ulianza kwa kikundi cha watu wasiozidi 15 kupitia Mtandao wa Vikundi
vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) katika mkutano wa kimkakati uliofanyika
katika Chuo cha Ushirika tawi la Shinyanga, mwezi Septemba mwaka 2010.
Miongoni mwao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa mtandao kwa Wilaya ya Shinyanga
Vijijini, Titus Ndugulile kutoka kijiji cha Mwamala.
“Ni
vigumu kuamini kama mpango huu umekuwa mkubwa kiasi hiki. Tulianza watu
12 tu miaka mitano iliyopita, lakini leo tupo waraghbishi zaidi ya 400.
Kwa hakika haya ni mafuriko ya waraghbishi, kwani sasa kila sehemu
wanapatikana,” alisema Ndugulile.
Viongozi
wa mitandao ya wilaya za Bukombe na Mbogwe mkoani Geita wakiwa katika
kikao cha pamoja kilichofanyika katika kata ya Masumbwe hivi karibuni
|
Baada
ya kikao hicho, yalifuata mafunzo maalumu ya uraghbishi kwa siku tatu
yakiendeshwa kila wilaya. Mafunzo hayo yalilenga kufundisha namna ya
kutafuta na kupata taarifa na kutambua changamoto zinazoikabili jamii na
njia za kuzitatua.
“Nilikwenda
ofisi zetu za halmashauri kuulizia vyanzo vya mapato vya wilaya na
kuelezwa kuwa Mgodi wa Mwadui hauchangii chochote pamoja na kuwa upo
katika eneo hilo. Taarifa hii niliwashirikisha na wenzangu pia.”
Mraghabishi toka kijiji cha Negezi wilayani Kishapu Fredina Said amekuwa chachu ya maendeleo katika kijiji chake
|
Hayo ni maneno ya mraghbishi Fredina Said kutoka kijiji cha Negezi, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Pamoja na kwamba hakuweza kulifikisha mbali suala hilo, angalau aliweza kufahamu kilichokuwa kikiendelea.
Pamoja
na mambo hayo, walifundishwa pia namna ya kujiamini kupitia mafunzo ya
uraghbishi waliyokuwa wakiyapata kwa mara ya kwanza. Mafunzo haya
yalitolewa kwa nadharia na vitendo ambapo waraghbishi baada ya kupatiwa
mafunzo ya darasani walipewa kazi ya kutembelea ofisi za halmashauri za
wilaya zao.
Lengo
ni moja tu, kuwajengea uwezo wa kuongea na viongozi wa kitaifa kama
mkuu wa wilaya au mkurugenzi baada ya awali kuonyesha hofu na
kutojiamini.
“Ilikuwa
mara ya kwanza kuonana na mkuu wa wilaya na kumuulizia masuala ya
pembejeo za kilimo. Nilikuwa na hofu, hata hivyo kinyume na matarajio
yangu, maswali yote aliyajibu ingawa siyo kwa kiwango nilichotarajia,”
alisema mraghbishi Fedson Yaida wa Kijiji cha Shenda, wilaya Mbogwe,
mkoani Geita.
Matokeo ya kutembelea ofisi hizo yalionekana pale walipopatiwa majibu ya maswali yao.
Kazi
hii ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kuwandaa waraghbishi na majukumu
makubwa ya uraghbishi. Waraghbishi hawa walikuwa wakiwakilisha wananchi
wa vijiji vyao, hivyo moja ya jukumu lao ilikuwa ni kuwashirikisha
walichojifunza.
Jukumu hilo walilifanya vizuri na waliweza kutambuliwa kwa urahisi na viongozi wa vijiji pamoja na wananchi wenzao.
Na
kwa sababu walipatiwa mafunzo kupitia mradi wa Chukua Hatua, walijikuta
wakiitwa kwa jina hilo hilo la Chukua Hatua. Mfano mzuri ni waraghbishi
waliopo katika kijiji cha Mwime, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hali
hii ilisababisha wananchi wengi katika vijiji ambavyo mradi wa Chukua
Hatua unaendeshwa kujitambulisha kama waraghbishi na kutaka na wao
wapatiwe mafunzo. Na hapo ndipo lilipokuja wazo la kuwawezesha
waraghbishi wa zamani na wapya kufanya kazi kwa pamoja.
Mraghbishi kutoka Kijiji cha Ololosokwani, Kootu Tome,akigawa majarida yenye riwaya za za chukua hatua kwa wanakijiji wenzake
|
Akielezea
jinsi alivyowafundisha waraghbishi jinsi ya kufanya uraghbishi katika
kijiji chake na vile vya jirani, mraghbishi kutoka Kijiji cha
Ololosokwani, Kootu Tome, alisema:
“Nimefundisha
waraghbishi wa kijiji cha jirani. Niliwaeleza maana ya uraghbishi,
kwamba hawatakiwi kujionyesha wazi kwa kila jambo, badala yake
wanawashawishi watu kuchukua hatua katika kile anachokuwa
amewafafanulia,”
Mraghbishi
mwingine ni Julius Katende kutoka Kijiji cha Ngarwa, wilayani
Ngorongongo aliwafundisha waraghbishi wapya tofauti ya uraghbishi na
uhamasishaji. Mraghbishi si mwamasishaji, bali ni mtu anayeibua hoja
katika jamii na kuzitafutia majibu kwa kushirikiana na wenzake.
Jumla
ya waraghbishi wapya 762 wamefundishwa na waraghbishi 322 wa zamani,
ikiwa ni ongezeko mara mbili katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia
mwezi Julai hadi Septemba na kufanya idadi yao kuwa 1,084. Kati yao,
wanawake ni zaidi ya 400. Hili ni ongozeko kubwa ambalo ni wazi
linatokana na juhudi za pamoja.
“Tuliwafundisha
kutoka katika maeneo mbalimbali ambayo wamekuwa na kawaida ya
kukusanyika,” haya ni maneno ya mkurugenzi wa Tamasha, Richard Mabala,
wakati akifafanua namna wanavyoendesha mafunzo hayo katika mikoa ya
Kanda ya Ziwa.
Waraghbishi
kwa upande mmoja wanawakilisha wananchi wa maeneo yao na wamekuwa
mstari wa mbele kusimamia rasilimali zao na kuhakikisha huduma bora za
jamii zinapatikana. Lakini ili kufanikisha, malengo ya mpango wa Chukua
Hatua, viongozi wa vijiji, hasa wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji
wanafundishwa uraghbishi pia kulingana na nafasi zao.
Mkurungezi
wa CABUIPA David Rwegoshora akifafanua jambo katika mkutano
uliokutanisha waragahbishi toka mikoa ya Shinyanga ,simiyu na Arusha
|
Jukumu
la kuwafundisha viongozi hawa kwa upande wa mikoa ya kanda ya ziwa
wamepewa CABUIPA, shirika mdau la mpango wa Chukua Hatua lilipo Kahama.
Akifafanua wanachofanya, mkurugenzi wa shirika hilo, David Rwegoshora
alisema:
“Katika kipindi cha miezi mitatu tumefundisha wenyeviti 167 na watendaji 33 ngazi ya kata. Kati yao, wanawake walikuwa sita.”
Waraghbishi
toka kijiji cha Pandagichiza wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya
tanki la maji, ambalo baadhi yao ndio wasimamizi wake kutokana uaminifu
wao
|
Kwa
upande wa Ngorongoro, wenyeviti 14, watendaji 14 wa vijiji na 6 wa kata
walipatiwa mafunzo hayo. Kundi lingine ni Sungusungu, ambapo hadi sasa
idadi yao ni 15 nao walipewa mafunzo hayo ya uraghbishi. Wote hawa ni
waraghbishi kwa nafasi zao. Katika awamu iliyopita ilijumuisha na
viongozi wa dini wakiwamo masheikh, maimamu, wachungaji na makatekista.
Katika
kuhakikisha waraghbishi wanawafikia watu wengi zaidi na kuwafundisha
uraghbishi, mitandao ya waraghbishi imeanzishwa katika wilaya za Mbogwe,
Kahama, Maswa, Kishapu, Bariadi, Shinyanga Vijijini, Itilima na
Bukombe. Mitandao hii ilianza rasmi mwaka 2014 na kuwaleta pamoja
waraghbishi wa mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.
Hadi
sasa, kuna wenyeviti pamoja na wasaidizi wao, ambao idadi yao imefikia
32, wanawake 16, sawa na asilimia 50. Wingi huu wa waraghbishi
hauangalii itikadi za vyama, badala yake unaangalia kilicho bora kwa
wanajamii kwa ujumla.
Post a Comment