NA; YOHANA CHANCE.
ARUSHA.
Timu ya AFC inayoshiriki ligi daraja la pili (SDL) ilipata
ajali wiki iliyopita Mkoani wiki Singida ikiwa inaelekea Mkoani Shinyanga kwenye
nchezo wa mwendelezo wa ligi hiyo dhidi ya Bulyanhuru.
Katibu msaidizi wa timu hiyo Charles Mwaimu Alisema kuwa ajali
hiyo ilitokea maeneo ya Nanga Mkoani Singida hivyo kufanya wachelewe kufika
uwanjani.
“tunamshukuru Mungu hakuna mtu hata mmoja aliyeumia japo kuna
baadhi yetu walipata maumvu sehemu mbalimbali za miili yao ila mambo mengine
yalienda sawa,maana tulitoa taarifa mara baada ya kutokea tatizo hivyo mchezo
wetu ulichelewa kuanza” alisema Mwaimu.
Mchezo huo ulihairishwa mara mbili ambapo ulikuwa ucheze
jumapili iliyopita ikashindika kutokana na kuwepo kwa Shinyanga Dabi kati ya
Mwadui na Standi United.
Pia ulipendekezwa ucheze siku ya jumatatu wiki hii hivyo
uongozi wa AFC ulipeleka Maombi TFF Kuomba mchezo upelekwe tena mbele kutokana
na kuwepo kwa uchaguzi wa ubunge jimbo la Arusha jumapili iliyopita, hivyo
mchezo huo ulichezwa siku ya jumanne.
Katika
mchezo huo AFC walipoteza kwa kufungwa Mabao 3-0 hivyo
kujikuta wkipoteza michezo yote ya SDL huku mchezo uliopigwa mwishoni
mwa wiki walicheza na Madini Fc Katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid na
kutoka sare ya bao 1-0.
Post a Comment