NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA
Ligi daraja
la tatu ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kuendelea tena leo jumatatu kwa michezo kadhaa Kuchezwa
ili kusaka nafasi ya kuingia sita bora ya ligi hiyo.
Timu ya
Mvuleni itachez na Lang’ata katika uwanja wa Magereza, Kilimanjaro Fc
wataikaribisha Machame United katika uwanja wa Jamuhuri, wakati katika uwanja
wa Ushirika timu ya Kitoyosa watacheza na Ushirika Fc.
Ligi hiyo
inajumuisha timu kutoka wilaya na Manispaa zote zilizokuwa ndani ya Mkoa wa
Kilimanjaro ikiwemo Wilaya ya Hai, Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha,Vunjo na
Rombo
Katibu Mkuu wa
chama cha Soka Mkoani humo Mohamed Musa, alisema ligi hiyo inajumla ya timu 18
ambazo zigawanywa makundi mawili, huku kila kundi likiwa linatimu tisa.
Katika kundi
la kwanza kuna timu ya Afro Boys, Kilimanjaro Fc, Reli Manispaa, Ushirika
United, Kitayosa FC, Machame United,nyingine ni pamoja na KIA Sc, Machava na
Sango Fc.
Kundi B
limebeba timu ya Lang’ata, Hai, Forest Fc, Mvulen , New generation, Pozolana,
Upendo FC, Soweto united na Kilimanjaro Rangers.
Kila kundi
litatoa timu tatu ambazo zitaingia hatua ya Sita bora itakayoaanza januari 3
mwaka ujao ili kumpata Bingwa Wa Mkoa Atakayewakilisha Mkoa huo kwenye ligi ya
Mabingwa wa Mikoa.
Post a Comment