Na; Yohana Challe
ARUSHA.
Timu ya JKT
Oljoro imetolewa katika michuano ya FA inayoendelea hapa nchini, baada ya kukubali
kufungwa na timu ya Mdini FC inayoshiriki ligi daraja la Pili kwa mikwaju ya
penati 7-6, mchezo uliochezwa ktika uwanja wa Sheikh Amri Abeid juzi jumatano.
Hatua ya
Mikwaju ya Penati ilikuja baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bila kufungana
ndipo mikwaju ya penati ikamuliwa kupigwa.
Waliopiga penati
kwa upande wa Oljoro ni Paulo Malipesa, Lawrence Milton, Shaibu Nayopa, Swalehe
Hussein, Abdul Ibadi, Said Mashaka wote wakiwa wamefunga penati zao wakati
Lucas Charles Mkwaju wake uliota mbawa baada ya kudakwa na Golikipa wa Madini
Sebashar Stanley.
Kwa upande
wa timu ya Madini walioipa ushindi timu hiyo baada ya kupiga mkwaju yao na
kupata zote ni pamoja na Wilson Mollel, Edward Kang’ori. Ramadhan Ntobi, Lesika
Lekindoki, Fred Paulo, Juma Juma na Priscus Julius.
Mara baadaya
ya mchezo huo Kocha wa JKT Oljoro Joery Mwambegele alisema kuwa bahati haikua
yao, hivyo kwa sasa wanaelekeza nguvu kwenye ligi daraja la kwanza hasa
mzunguko wa pili utakaonza Mwishoni mwa mwezi huu.
Post a Comment