PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Habari picha -Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Wiliam Ole Nasha akishukuru kwa uteuzi wa JPM
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Wiliam Ole Nasha akishukuru kwa uteuzi wa Rais John Pombe Magufuli  katika baraza la Madiwani wa ...
Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Wiliam Ole Nasha akishukuru kwa uteuzi wa Rais John Pombe Magufuli  katika baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ,Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda,Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Hashim na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mathew Siloma.Picha na Ferdinand Shayo

Naibu Waziri Mteule wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  William Ole Nasha amesema kuwa hatamwangusha Raisi John Pombe Magufuli na Watanzania kwa kuhakikisha kuwa anawajibika na kufanya kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko katika sekta hizo .

Nasha ambaye uteuzi  huo ulivyotangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari ulimkuta katika Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro hali iliyowashangaza wengi kwani hawakuwa wametarajia kuwa uteuzi huo ungetokea.

Akizungumza katika baraza la Madiwani Nasha alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuwa hatawaangusha Watanzania  kuwa hana rekodi ya kukosa maadili.

“Umakini mkubwa umetumika kuteua baraza la Mawaziri mpaka leo hii Mheshimiwa Raisi hajamaliza kuteua baraza , ni heshima kubwa sana kwangu namshukuru Magufuli kwa dhamana hii kubwa “ Alisema Nasha

Nasha amesema kuwa atashirikiana na wataalamu kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika taifa la Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda ambaye alikuwepo wilayani hapo katika ziara yake ya kikazi ya siku 3 amempongeza Mbunge huyo wa Ngorongoro ambaye kwa sasa ni Mbunge Mteule wa Ngorongoro.

Ntibenda amesema kuwa anaamini kupitia uteuzi huo utasaidia kuinua sekta ya ufugaji kutoka kwenye ufugaji wa kienyeji hadi kwenye ufugaji wa kisasa utakaoleta tija na kuinua uchumi wa wafugaji na taifa kwa ujumla.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top