Ndugu Wasamaria wema,
UPDTAES ZA LEO
Kwa
kutumia michango ya wasamaria wema, leo tayari Ankal ameshalipia malipo
kwa ajili ya vipimo vya MRI kwa dada Joyce yanayotarajiwa kufanyika
Alhamisi hii ama Ijumaa. Baada ya matokeo ya vipimo vyake jopo la
madaktari bingwa bingwa litakaa nakuamua nini cha kufanya kumsaidia dada
Joyce. Hivyo tuendelee kumsaidia kwa hali na mali pamoja na dua.
Kama umeguswa na unataka kutoa msaada unaweza kuwasiliana na Ankal kwa email issamichuzi@gmail.com am a whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.
AU mratibu-mwenza Deo Kakuru Msi mu
Pia unaweza kuwasiliana moja
kwa moja na dada Joyce kwa namba hiyo na atafurahi
ukimsalimia ama hata kumtupia kitu kwenye Mpesa yake.
MPIGIE +255 768 084897
------------------------------ -----------
HISTORIA YA MATATIZO YA DADA JOYCE
Ifuatayo
ni historia fupi ya matatizo ya dada Joyce Richard Mwambepo, mkaazi wa
kitongoji cha Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi
na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa
miaka 4.
Ikumbukwe
kuwa mwezi wa nne (April) mwaka jana dada huyu aligongwa na gari ambalo
dereva wake hakusimama kumsaidia. Wasamaria wema walijitokeza na
kumpelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako alikaa wodini kwa
miezi mitatu bila kupata matibabu kwa kukosa fedha.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini nako huko pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya kwa kukosa pesa za matibabu.
Akajitokeza
mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya ambaye baada ya kumgundua alitoa
taarifa za dada Joyce katika mitandao mbalimbali, ambapo wasamaria wema
wengi wa ndani na nje ya nchi wakaguswa na kuchangia.
Mungu
mkubwa, kiasi kilichopatikana ( 3.2m/-) kimewezesha dada Joyce
kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya Fast Jet Alhamisi
iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ambako alipokelewa katika kitengo cha mifupa cha MOI na kupatiwa kitanda
katika wodi mpya ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu
wodi namba 2 chumba cha kwanza kulia.
Cha
kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na
hata kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema
limemsaidia kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea
taratibu na ukimgusa anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.
Daktari
bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya
chini ya uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea
kubana mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze. Zoezi linalosubiriwa
kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha tatizo lake
na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika wakati
wowote kuanzia sasa.
Mpiganaji
Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce
amekabidhiwa Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na
kumsaidia kwa hali na mali dada huyu ambaye ni yatima.
Kwa
bahati njema Ankal amekutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye
Mama Rozi ambaye anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa wodi moja na
dada Joyce. Msamaria huyu amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na
pia kumsaidia usafi maana hapo kitandani alipo hawezi kuondoka...Hivyo
mambo yote anamalizia hapo hapo.
Mungu
kweli ni mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa
shukurani sana kwa wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema
hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba
awazidishie pale patapopungua. Ameomba anayeweza kumtembelea afanye
hivyo na atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam zaidi ya
Ankal.
Pia
anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao mkubwa
waliompa wakati wa kupata ajali na huu.
Dada
Joyce pia anawashukuru sana Dkt Hellen na Dkt Mtei ambao amesema
wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba huduma anazopata hapo
MOI ni zitamsaidia kupata matibabu yake.
Hati
ya malipo kwa ajili ya vipimo vya MRI kwa dada Joyce iliyotolewa leo
baada ya kulipiwa. Inatarajiwa atapimwa Alhamisi ama Ijumaa kabla jopo
la Madaktari kuamua nini cha kumfanyia.
Mpiganaji Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya kuelekea Dar es salaam Alhamisi iliyopita.
Dada Joyce akiwa ameketi kwa utulivu kwenye siti yake ndani ya ndege wakati wa safari ya kutoka Mbeya kuelekea Dar es salaam.
Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam
Msamaria
mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo
kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu
Dada Joyce akiwa wodini Moi
Post a Comment