PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BAYI AWAPONGEZA WANARIADHA ARUSHA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amewapongeza wanariadha walioshiriki mash...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amewapongeza wanariadha walioshiriki mashindano ya Kutangaza utalii wa ndani yaliyofanyika mwishoni mwa Wiki jijini hapa yakishirikisha wanariadha kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Bayi alisema kwa kushiriki kwao katika mashindano mengi ya mchezo huo yatawatengenezea njia ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuitangaza upya Tanazania kupitia mchezo huo kama ilivyokua enzi zao.

“wanariadha wetu ni walewale na hakuna wengine na siku chache zilizopita walikuwa Babati kwenye mashindano pia, hivyo kuwepo kwa mashindano mengi itamsaidia sana kujua uwezo wake kwa kuangalia muda anaotumia na pia nafasi anayomaliza kwa kila shindano, mfano akimaliza nafasi tano za juu katika mashindano saba inamaa atakuwa ameongeza kitu”alisema Bayi.

Aliongeza kuwa inatakiwa watu wafahamu ya kwamba sio kila mashindano yaitwe Marathoni maana halisi ya neeno marathoni kwa kigiriki inamaana kilometa 42 lakini ameshuhudia mashindano mengi yakiitwa jina hilo pasipo kuwepo na uhalisia.

“kuna Mashindano ya Kilimanjaro,Serengeti, na yale ya rock, waandaaji wanayaita Marathoni nadhani inatakiwa elimu ya hali ya juu hapo, km 21 huwezi kuita Marathon” Alisema Bayi.

Kwa Upande wake Fabian Joseph ambaye alishiriki mashindano hayo na kumaliza nafasi ya Pili alisema kuwa mashindano hayo yanalejesha ile hali ya kimichezo ya Arusha baada ya kupotea kwa muda mrefu.

Riginal Lucian alishika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo wakati Fabiani Joseph akimaliza nafasi ya Pili na nafai ya Tatu ikaenda kwa Gabriel Gerald, na Evance Kiblang’ata kutoka Kenya Alishika nafasi ya nne.

Kwa upande wa Wanawake Angelina Tsere kutoka Nchini Kenya aliweza kumaliza katika nafasi ya Kwanza huku Mary Naali wa Tanzania alishika nafasi ya pili na Ladis Shemayo raia wa Kenya alikuwa wa Tatu

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top