NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Katibu mkuu
wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amewapongeza wanariadha
walioshiriki mashindano ya Kutangaza utalii wa ndani yaliyofanyika mwishoni mwa
Wiki jijini hapa yakishirikisha wanariadha kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Bayi alisema
kwa kushiriki kwao katika mashindano mengi ya mchezo huo yatawatengenezea njia
ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuitangaza upya Tanazania
kupitia mchezo huo kama ilivyokua enzi zao.
“wanariadha
wetu ni walewale na hakuna wengine na siku chache zilizopita walikuwa Babati
kwenye mashindano pia, hivyo kuwepo kwa mashindano mengi itamsaidia sana kujua
uwezo wake kwa kuangalia muda anaotumia na pia nafasi anayomaliza kwa kila shindano,
mfano akimaliza nafasi tano za juu katika mashindano saba inamaa atakuwa
ameongeza kitu”alisema Bayi.
Aliongeza
kuwa inatakiwa watu wafahamu ya kwamba sio kila mashindano yaitwe Marathoni
maana halisi ya neeno marathoni kwa kigiriki inamaana kilometa 42 lakini
ameshuhudia mashindano mengi yakiitwa jina hilo pasipo kuwepo na uhalisia.
“kuna
Mashindano ya Kilimanjaro,Serengeti, na yale ya rock, waandaaji wanayaita
Marathoni nadhani inatakiwa elimu ya hali ya juu hapo, km 21 huwezi kuita
Marathon” Alisema Bayi.
Kwa Upande
wake Fabian Joseph ambaye alishiriki mashindano hayo na kumaliza nafasi ya Pili
alisema kuwa mashindano hayo yanalejesha ile hali ya kimichezo ya Arusha baada
ya kupotea kwa muda mrefu.
Riginal Lucian
alishika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo wakati Fabiani Joseph
akimaliza nafasi ya Pili na nafai ya Tatu ikaenda kwa Gabriel Gerald, na Evance
Kiblang’ata kutoka Kenya Alishika nafasi ya nne.
Post a Comment