NA; YOHANA CHALLE
ARUSHA.
Chama cha Riadha
mkoa wa Arusha (ARAA) ,kimeanza maandalizi ya msimu mpya wa mbio za Nyika
(Cross Country) katika kuwajenga wanariadha kujiwekea nafasi bora ili waweze
kuteuliwa kuingia katika timu ya taifa ya mchezo huu.
Katika ufunguzi
wa mbio hizo zilizofanyika katika eneo la Magereza jijini hapa
uliwakutanisha wanariadha 12, huku kati yao mwanamke
akijitokeza mmoja, ambao watakabiliwa na michezo mingine mbele kwa ajili ya
kujinoa Zaidi.
Mapema January 9 wanariadha
watakwenda Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mashindano mengine yatakayofikia
tamati ifikapo March 12, 2016 ndipo wanariadha hao watakuwa tayari
wamejiongezea Pointi.
Katika mbio hizo
wanawake na wanaume waliweza kukimbia km 10 na Panuel Mkungo
kutoka klabu ya holili – Moshi aliweza kushika nafasi ya kwanza
baada ya kutumia muda wa dakika 31 :24:16,nafasi ya pili ilikwenda kwa
Faraja Lazaro kutoka pia klabu ya Holili -Moshi aliyetumia muda wa
dakika 32:37:82 na Yohana Elisante kutoka Arusha alishika
nafsi ya tatu baada ya kutumia muda wa dakika 33:37:88.
Kwa wanawake
ilikuwa ni km 8 lakini Bertha Marco ndiye mwanamke ekee aliyeshiriki na
alifanikiwa kutumia muda wa dakika 32:14:90.
Mratibu wa mbio
hizo Francis John alieleza kuwa wameanza kuwaweka vijana wawe katika uwezo
mzuri kwa ajili ya baadae ili waweze kuteuliwa kuingia timu ya taifa itakayo
shiriki mashindano ya mbio za nyika ya dunia yatakayofanyika jijini
Kampala nchini Uganda ifikapo mwaka 2017.
“Tumeanza msimu
mpya wa mbio hizi ambapo wanariadha kutoka mikoa miwili ya Arusha na
Kilimanjaro ndio wameweza kujitokeza na kushiriki licha baadhi ya vilabu vya
riadha hasa vya majeshi kushindwa kujitokeza kutokana na kuwa kazi
ulinzi kwa mujibu wa taarifa tuliyopata” alisema John.
Mbio hizo
zimeandaliwa na kamati ndogo ya mbio za Nyika (Cross Country) huku mbio
za barabarani zinatarajia kufanyika kwa msaada wa chama cha riadha Taifa (RT).
Post a Comment