Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.
Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Lenye makao
yake makuu jijini Paris, Ufaransa kupitia Mkurugenzi wake Mkuu limetoa
ripoti ya ujumbe wake kuelekea siku ya Sayansi Duniani kwa amani
inayotarajia kuadhimishwa leo hii Novemba 10, Duniani kote.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO , Bi Irina Bokova, katika ujumbe wake, juu ya maadhimisho ya leo ameweza kugusia mambo mbalimbali:
"Hii
Siku ya Sayansi Duniani kwa Amani na Maendeleo imekuja miezi miwili
baada ya makubaliano ya Agenda 2030 ya maendeleo endelevu.
Ajenda
hii mpya inajumuisha maono mapya kwa binadamu, kwa dunia, kwa amani ,
kwa miaka 15 ijayo na sayansi inasimamia katika moyo wake kama kichocheo
cha mageuzi chanya na maendeleo.
Serikali
zote kwa ujumla zinatambua leo nguvu ya sayansi ya kutoa majibu muhimu
kwa usimamizi mzuri wa maji, kwa ajili ya hifadhi na matumizi endelevu
ya bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe hai, ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi na majanga, na kuendeleza uvumbuzi na
kuondokana umaskini na kupunguza tofauti .
Kufanya haya, tunahitaji kuelewa wazi zaidi mazingira ya kimataifa ya sayansi na tunahitaji zana bora kufuatilia maendeleo .
Huu
ndio umuhimu wa ripoti ya Sayansi ya UNESCO, inayotolewa kila miaka
mitano, inayotoa mwenendo wa sayansi, teknolojia na uvumbuzi katika
kila kanda.
Tutazindua
toleo jipya katika Siku ya Sayansi Duniani kwa ajili Amani na
Maendeleo 2015, kuonyesha mwelekeo wa sayansi, teknolojia na maendeleo
kwa kila nchi katika ngazi zote za maendeleo. Kuongezeka kwa wasiwasi wa
ukame, mafuriko, vimbunga na matukio mengine ya asili yamesababisha
Serikali kupitisha mikakati katika ngazi za kitaifa na kikanda kulinda
kilimo, kupunguza hatari ya maafa na kuongeza vyanzo vya kitaifa vya
nishati.
Kuongezeka
kwa uwekezaji katika sayansi huonyesha kutambuliwa zaidi haja ya
kujenga jamii na uchumi wa kijani, kuleta mabadiliko katika sera na
sheria ikiwa ni pamoja na maadili na tabia.
Maswali
haya yatashughulikiwa katika mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa wa
Mabadiliko ya Tabianchi ( COP21 ) utakaofanyika Paris mwezi ujao, wakati
viongozi kutoka pande zote za dunia watakapokusanyika kupitisha mkataba
mpya wa ushirikiano wa kimataifa wa kukabiliana na madhara ya
mabadiliko ya tabia nchi.
Sayansi,
teknolojia na ubunifu ni muhimu hapa, na ni lazima tufanye kila kitu
kusaidia jamii zote duniani, kujenga na kubadilishana maarifa. Agenda ya
2030, pamoja na ajenda ya maamuzi ya Addis Ababa, imetoa wito kujenga
sera imara za kitaifa za sayansi, teknolojia na ubunifu pamoja na
mifumo, ili kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na ubunifu, ambayo UNESCO
imejizatiti kamilifu .
Huu
ni ujumbe wa Ripoti ya Sayansi ya UNESCO na hii Siku ya Sayansi Duniani
kwa Amani na Maendeleo. Nawakaribisha wote kujiunga na sisi katika
kuuchukua huu ujumbe duniani kote na kujenga maisha bora ya baadaye kwa
wote " Alimalizia Mkurugenzi Mkuu huyo.
Kwa habari zaidi ya ripoti hii inapatikana katika tovuti ya UNESCO ; http://www.unesco.org
Kwa maelezo zaidi unaweza pia kuwasiliana na Ofisi ya UNESCO iliyopo karibu nawe, na kwa Dar es Salaam kupitia: barua pepe: dar-es-salaam@unesco.org au tovuti: http://www.unescodar. or.tz na mawasiliano ya ofisi Simu ya Ofisi: +255 22 2915400
Post a Comment