NA;
YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Ofisa mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Boniface Wambura amesema kuwa Timu za Ligi daraja
la kwanza zinatakiwa kujirekebisha mapema kabla ya mzunguko wa pili kuanza.
Wambura Alisema
hayo jijini Arusha alipohudhulia mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya JKT
Oljoro na Polisi Tabora, huku akiwa anasisitiza kuwa ligi hiyo itaanza
kuoneshwa kwenye Televisheni pindi mzunguko wa Pili utakapoanza, hivyo kuna
baadhi ya makosa yanaonekana ambayo sio sahihi kwa Timu za ligi daraja la
kwanza kuzifanya.
“Nimefanya
uchunguzi kwenye michezo kadhaa ya ligi hii na nimegundua dakika za mwisho
waokotaji wa mipira (Ball Boys) wanakuwa wameshaondoka jambo ambalo sio
sahihi,kwa kuwa wanatakiwa kuondoka uwanjani pindi mchezo unapoisha”alisema
Wambura.
Aliongeza kuwa
kuna vitendo ambavyo havifai kufanywa kwenye mchezo, kwa kuwa ni kinyume na
taratibu na sheria za kisoka kwa kuwa zinashusha hadhi ya timu na ligi pia,
japo timu husika inaamini inasaidia kupoteza muda.
Wambura alisema
kuwa Timu nyingi za ligi daraja la kwanza hazina uhamasishaji, tofauti na zile
zilizokuwa ligi kuu, hivyo Bodi ya ligi imejiandaa kukaa na viongozi wa timu
ili kuliangalia suala hilo kabla ya kipute cha mzunguko wa pili kuanza.
“Wasiitazame TFF
au ya Bodi ya ligi, unapokuwa mwenyeji katika mchezo unatakiwa ufanye
uhamasishaji ili watazamaji waje kwa wingi kwa kuwa mapato yanayopatikana
uwanjani wenyeji ndio wanaopata asilimia kubwa ya mapato kuzidi mgeni”.
“Mwezi ujao tunatarajia
kufanya semina na maofisa Habari na maofisa masoko wa timu zote zinazoshiriki
ligi daraja la kwanza ili tuwasaidie jinsi ya kupata wadhamini watakaowaidia
katika timu zao” alisema Wambura.
Wachezaji na
watazamaji wamekumbushwa kuzingatia sheria za michezo hasa kwenye michezo
inayohusisha timu za Jeshi au Polisi zimeonekana kuvunja Sheria kila wakati
jambo ambalo sio zuri kwa wanamichezo.
Post a Comment