PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JKT OLJORO, PANONE FC ZATUNISHIANA KIFUA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya JKT Oljoro ya Arusha na Panone FC ya mkoani Kilimanjaro,ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya JKT Oljoro ya Arusha na Panone FC ya mkoani Kilimanjaro,ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza ngazi ya Taifa (FDL), zimeanza kutunishiana kifua kila mmoja akiahidi kupanda ligi kuu msimu ujao.

Mwishoni mwa wiki hii Timu hizo zinashuka dimbani baada ya ligi kusimamishwa kupisha zoezi la upigaji kura, JKT Oljoro watakuwa Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakiikaribisha Geita Gold Stars.

Wakati  Oljoro wakiikaribisha Geita, nayo Panone FC maalufu kama matajiri wa mafuta wao watakuwa katika uwanja wao wa ushirika wakiikaribisha Polisi Mara.

Msemaji wa Panone FC Cassim Mwinyi alisema kuwa tayari kikosi kinaendelea kujiimalisha kuelekea mchezo wa jumamosi dhidi ya Polisi Mara.

“wapenzi wa Panone wasiwe na wasiwasi kwani tuna kikosi imara cha wachezaji 27 na wote wanania moja, hivyo mchezo wa jumamosi ni kama fainali kwetu” alisema Mwinyi.

Katika mchezo wa mwisho Panone walipata ushindi ugenini wa bao 2-1dhidi ya Mbao FC.

Naye katibu mkuu wa JKT Oljoro Hussein Nalinga, alisema kuwa wanamatumaini makubwa kushinda katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Geita kutokana na uimara wa kikosi chake japo wataingiauwanjani kwa tahadhari kubwa kutokana na ushindani unaoneshwa na Geita katika michezo ilipita.

Katika kundi hilo msimamo unaonesha Geita anaongoza kwa pointi 9, Polisi Tabora Pointi 8 sawa na JKT Oljoro zikitofautiana kwa magoli matatu.

Nafasi ya nne imekaliwa na Panone Fc yenye Pointi 7 sawa na Rhino Rangers,na Mbao FC, Nayo Polisi Mara ikishika nafasi ya saba na kujikusanyia Pointi 5 na Kanembwa JKT ikiburuza mkia Katika kundi hilo ikiwa na Pointi 1.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top