NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu ya JKT
Oljoro ya Arusha na Panone FC ya mkoani Kilimanjaro,ambazo zinashiriki ligi
daraja la kwanza ngazi ya Taifa (FDL), zimeanza kutunishiana kifua kila mmoja
akiahidi kupanda ligi kuu msimu ujao.
Mwishoni mwa
wiki hii Timu hizo zinashuka dimbani baada ya ligi kusimamishwa kupisha zoezi
la upigaji kura, JKT Oljoro watakuwa Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
wakiikaribisha Geita Gold Stars.
Wakati Oljoro wakiikaribisha Geita, nayo Panone FC
maalufu kama matajiri wa mafuta wao watakuwa katika uwanja wao wa ushirika
wakiikaribisha Polisi Mara.
Msemaji wa
Panone FC Cassim Mwinyi alisema kuwa tayari kikosi kinaendelea kujiimalisha
kuelekea mchezo wa jumamosi dhidi ya Polisi Mara.
“wapenzi wa
Panone wasiwe na wasiwasi kwani tuna kikosi imara cha wachezaji 27 na wote
wanania moja, hivyo mchezo wa jumamosi ni kama fainali kwetu” alisema Mwinyi.
Katika mchezo
wa mwisho Panone walipata ushindi ugenini wa bao 2-1dhidi ya Mbao FC.
Naye katibu
mkuu wa JKT Oljoro Hussein Nalinga, alisema kuwa wanamatumaini makubwa kushinda
katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Geita kutokana na uimara wa kikosi chake
japo wataingiauwanjani kwa tahadhari kubwa kutokana na ushindani unaoneshwa na
Geita katika michezo ilipita.
Katika kundi
hilo msimamo unaonesha Geita anaongoza kwa pointi 9, Polisi Tabora Pointi 8 sawa
na JKT Oljoro zikitofautiana kwa magoli matatu.
Nafasi ya
nne imekaliwa na Panone Fc yenye Pointi 7 sawa na Rhino Rangers,na Mbao FC,
Nayo Polisi Mara ikishika nafasi ya saba na kujikusanyia Pointi 5 na Kanembwa
JKT ikiburuza mkia Katika kundi hilo ikiwa na Pointi 1.
Post a Comment